Header Ads

ad

Breaking News

DIWANI NYAMWIJA: DUMISHENI NIDHAMU

DIWANI wa Kata Ya Hananasif wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Wilfred Elias Nyamwija, amewataka wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi, kudumisha nidhamu kwa kuwa ndiyo msingi mkuu wa maadili mema ili kujenga jamii na taifa lenye maadili mazuri.

Nyamwija ameyasema hayo mapema akiwa mgeni rasmi katika mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa darasa saba wa Shule ya Msingi Hananasif.

Pamoja na mambo mengine, Diwani Nyamwija ameahidi kutoa udhamini kwa wanafunzi 10, watakaofanya vizuri kwa  kuwagharamia mahitaji yao wakati wa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani.

Mbali na udhamini kwa wanafunzi, diwani huyo ameahidi kutoa zawadi kwa walimu ambao masomo yao yatatoa ufaulu wa juu katika mitihani ya darasa la saba shuleni hapo.


No comments