Diwani Nassa ataka agizo la Ridhiwani lifanyiwe kazi
![]() |
Tunu Mpwimbwi, Diwani Viti Maalum Tarafa ya Kwaruhombo |
Na Omary Mngindo, Chalinze
DIWANI wa Kata ya Bwilingu Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, Nassa Karama, ameiomba halmashauri hiyo kulifanyia kazi agizo la Naibu Waziri wa Utumishi, Ridhiwani Kikwete (Mbunge), linalohusu kupakia na kushusha abiria kwenye eneo la Chalinze.
Nassa alitoa rai hiyo kwenye Baraza la kawaida la madiwani hao, chini ya Kaimu Mwenyekiti, Mussa Gama ambaye ni Diwani Kata ya Vigwaza, Mkurugenzi Ramadhani Possi na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdul Sharifu, alisema agizo hilo bado halijatekelezwa.
"Kwa niaba ya wana Bwilingu na wanaosafiri kwenye mabasi yanayopita eneo hili, nawasilisha kilio chao ambacho kilielezwa na mbunge wetu, Ridhiwani Kikwete, aliyetuomba utaratibu wa zamani uendelee huku kukiweka utaratibu utaowabana madereva wanaokwepa kwenda stendi kuu kulipa ushuru," alisema Nassa.
Aliongeza kwamba, kuna usumbufu mkubwa unaosababishwa na madereva kukataa kushusha au kupakia abiria maeneo yote ya Bwilingu kuanzia Mashine ya Mbao, kabla ya Polisi ukitokea Chalinze Mzee na maeneo mengine, badala yake abiria ashuke stendi kuu, ili linalalamikiwa sana na wananchi.
Aliongeza kuwa, "Tangu kuanza kwa Stendi Kuu, wenye magari wanakatazwa kushusha na kupakia abiria kitendo kinacholalamikiwa na wananchi wetu, niwaombe tutekeleze ushauri wa mbunge wetu, Ridhiwani Kikwete la kuruhusu abiria kushuka kwenye vituo vya awali, kisha magari yafike stendi kulipa ushuru," alisema Nassa.
Madiwani Ramadhani Mkufya (Kibindu), Ramadhani Biga (Talawanda), Mohamed Gelegeza (Mkange) na Anzeni Rajabu walilitaka baraza hilo kurekebisha baadhi ya changamoto zilizopo katika maeneo yao.
"Pale Kibindu changamoto zilizopo ukosefu wa Kituo cha Polisi, tupo mbali na Kituo cha Mbwewe, ukosefu wa vitendea kazi ofisi ya Kata, migogoro ya ardhi vijiji vya Kwamduma, Gole, Handeni, Kwakonje na Kimamba, upungufu wa watumishi, wodi ya wazazi kituo cha afya na nyingine," alisema Mkufya.
"Kwa niaba ya Diwani wa Msata naomba kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za serikali kuanzia Aprili hadi Juni, baadhi ya changamoto za wana Msata zinahusu upungufu wa walimu wa shule za msingi, msongamano wanafunzi katika sekondari, uchakavu wa miundombinu ya elimu, wafugaji wavamizi na machinjio," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Naye Diwani wa Kata ya Mkange, Mohamed Gelegeza, alisema; "Mkange tunakabiliwa na changamoto za msongamano wa wanafunzi wa shule msingi hasa Mkange, maji si ya uhakika, nyumba za walimu, shule za msingi na viwanja kutopimwa kwa wakati hivyo, kushamiri kwa ujenzi holela," alisema Gelegeza.
![]() |
Nassa Karama, Diwani Kata ya Bwiligu |
![]() |
Mussa Gama, Diwani Kata ya Vigwaza |
![]() |
Ramadhan Possi, Mkurugenzi Mtendaji |
![]() |
Ramadhan Diga, Diwani Kata ya Talawanda |
No comments