WAWILI WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI PWANI KWA KUKUTWA NA GUNIA NANE ZA BANGI


Watuhumiwa
hao walionaswa na Jeshi la Polisi wamefahamika kwa mjina Abraham
Michael mwenye umri wa miaka 31 mkaazi wa Jijini Dar es Salaam na
Godfrey Malakasuka mwenye umri wa miaka 21 mkaazi wa Kimara
waliokamatwa katika eneo la Ubena Zomozi wakitokea Mkoani Morogoro
kuelekea Jijini Dar es Salamaa.

Akizungumza
na waandishi wa habari Kamanda wa Mkoa wa Pwani ACP Jonathan Shanna
alisema kuwa watuhumiwa wamekamatwa na vidhibiti hivyo wanastahili
kupata adhabu kali pindi watakapofikishwa mahakamani.
No comments