WAKAZI WA ARUSHA WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA MKANDARASI
Mhandisi
Mshauri kutoka Kampuni ya Cheil Engineering Bw. Shin Soo akimueleza
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
(katikati) maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mchepuo (Arusha bypass),
inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4. Kushoto ni
Meneja wa TANROADS mkoa wa Arusha Mhandisi Johnny Kalupale.
Mafundi
wa Kampuni ya M/S Hanil-Jiangsu J/V wakiendelea na ujenzi wa moja kati
ya madaraja makubwa saba yanayojengwa katika barabara ya mchepuo (Arusha
bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4.
Meneja
wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Arusha Mhandisi Johnny
Kalupale (kulia) akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto) hatua mbalimbali za maendeleo
ya ujenzi wa barabara ya mchepuo (Arusha bypass), wakati Waziri huyo
alipoikagua, mkoani Arusha.

Moja
kati ya madaraja saba yanayojengwa katika barabara ya mchepuo (Arusha
bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4, jijini
Arusha.
Tingatinga
likiendelea na kazi ya ujenzi wa awali ya madaraja katika barabara ya
mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa
KM 42.4, jijini Arusha.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto)
akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya Cheil
Engineering Bw. Shin Soo (katikati)alipokagua maendeleo ya ujenzi wa
barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami
yenye urefu wa KM 42.4 jijini Arusha.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ametoa wito
kwa wakazi wa Arusha kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi wa Kampuni ya M/S
Hanil-Jiangsu J/V ili kuweza kukamilisha kwa wakati ujenzi wa barabara
ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu
wa KM 42.4.
Akikagua
mradi wa ujenzi wa barabara hiyo mkoani humo, Profesa Mbarawa amesema
kukamilika kwa barabara hiyo kutapunguza msongamano wa magari katikati
ya jiji hilo na hivyo kuvutia watalii na kukuza uchumi wa mkoa.
"Kukamilika
kwa barabara hii ya Arusha bypass kutapunguza kwa kiasi kikubwa
msongamano kwani magari makubwa ya mizigo yatatumia mchepuo huu na
kurahisisha huduma za usafirishaji jijini Arusha", amesema Waziri
Mbarawa.Ameongeza
kuwa Wizara yake itasimamia kwa ukaribu ujenzi wa barabara hiyo ili
ikamilike kwa wakati uliopangwa na viwango vinavyostahili
vilivyokubalika.
Aidha,
Prof. Mbarawa ameupongeza Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani humo
kwa usimamizi mzuri wa barabara ya Sakina-Tengeru KM 14.1 iliyokamilika
kujengwa kwa kiwango cha lami na kusisitiza kuitunza barabara hiyo ili
idumu kwa muda uliopangwa.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Barabara wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi),
Eng. Ven Ndyamukama, amesema Wizara kwa kushirikiana na TANROADS
itaendelea kuhakikisha barabara na madaraja yote nchini yanajengwa kwa
viwango vilivyopo kwenye usanifu wa kina (Detail design), na thamani ya
fedha inapatikana.
Naye,
Meneja wa TANROADS mkoa wa Arusha Mhandisi Johnny Kalupale,
amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuendelea kumsimamia mkandarasi huyo
ili akamilishe mradi kwa wakati kama walivyokamilisha ujenzi wa
barabara ya Sakina-Tengeru KM 14.1 na kwa ubora unaostahili.
Mhandisi
Kalupale, ameeleza changamoto zinazoikabili barabara hiyo kuwa ni wingi
wa udongo wa tifutifu na mfinyanzi na hivyo kulazimu Usanifu wa kina
wa barabara hiyo kurudiwa upya.
Ujenzi
wa Barabara ya Arusha bypass unatarajiwa kutumia zaidi ya shilingi
Bilioni 67 ikiwa ni ushirikiano wa fedha za Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB), na Serikali ya Jamhuri ya Tanzania na ujenzi wake utahusisha
madaraja makubwa 7, maboksi kalvari 55 na madaraja ya bomba 55.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments