Header Ads

ad

Breaking News

NAIBU SPIKA TULIA ZIARANI WILAYA YA RUNGWE, AZINDUA JENGO LA MALIWATO YA WANAWAKE HOSPITALI YA WILAYA YA RUNGWE

 Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akipanda mti na Mwanafunzi wa darasa la tano wa Shule ya Msingi Segera, Jackson Lusajo, wakati alipotembelea shule hiyo kukabidhi Vifaa vya ukarabati wa shule hiyo akiwa katika ziara yake Wilaya ya Rungwe jana Sept 20, 2017. Jumla ya miti 160 ilipandwa katika shule hiyo ikiwa ni sehemu ya kutunza mazingira. Picha zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO MEDIA)
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tukuyu, Ezekiel Manyemele, wakifunua kitambaa kuzindua Jengo la Choo cha wanawake katika Hospitali ya Makandana Wilayani Rungwe, jana Sept 20, 2017. Jengo hilo la Choo limegharimu zaidi ya Sh. milioni 50. 
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akipanda mti na Mwanafunzi wa darasa la Sita wa Shule ya Msingi Segera, Tunza Fred, wakati alipotembelea shule hiyo kukabidhi Vifaa vya ukarabati wa shule hiyo akiwa katika ziara yake Wilaya ya Rungwe jana Sept 20, 2017. Jumla ya miti 160 ilipandwa katika shule hiyo ikiwa ni sehemu ya kutunza mazingira.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akiangalia tofali, wakati alipotembelea shule ya Msingi Segera kukabidhi Vifaa vya ukarabati wa shule hiyo akiwa katika ziara yake Wilaya ya Rungwe.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, akimkabidhi tofali, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Segera, Fred Mfwea (wa pili kulia) na Diwani wa Kata ya Segera (katikati) wakati alipotembelea shuleni hapo kukabidhi Vifaa vya ukarabati wa shule hiyo akiwa katika ziara yake Wilaya ya Rungwe.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, akicheza muziki 'Ndiyo Maana Tenzele' wa asili wa kabila la Wasafa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Unyamwange, Julius Pascal, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya akiangalisha fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo cha afya Kata ya Isongole jana.
 Picha ya pamoja na wafanyakazi wa Hospitali ya Makandana
 Akikagua jengo hilo ndani
 Akizungumza na kina mama wa Rungwe
 Akisalimiana na mwanafunzi Tunza.
 Mwanafunzi akimwagilia mti baada ya kupanda
 Dk. Tulia akikagua madarasa ya shule ya Segera
 Mwalimu mkuu wa shule hiyo akizungumza
 Vijana wa Taasisi ya Tulia Trust
 Walimu na wanachi wa shule hiyo wakisikiliza hotuba ya Dk. Tulia.
 Dk. Tulia akizungumza
 Dk. Tulia akipokea mchango wa fedha sh. 300,000 kutoka kwa Mkurugenzi wa Patrick Mission High School, Ndele Mwaselela,  pia alitoa ahadi ya kuchangia bando 10 za mabati kwa shule hiyo.
 Akitoa zawadi ya hela kwa wanafunzi wa shule hiyo kwa ajili ya sukari
 Dk. Tulia akikabidhi fedha hizo kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo
Dkt. Tulia akipokea zawadi ya kuku kutoka kwa mwalimu wa shule hiyo, Caroline Kilongo. Picha zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO MEDIA)

No comments