Tamasha la utamaduni Tukuyu ni chachu ya kukuza na kuendelezu utamaduni nchini

Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante
Ole Gabriel (aliyevaa mashuka ya Kimasai), akizungumza mbele ya washiriki wa
tamasha la ngoma za jadi linaloratibiwa na Taasisi ya Tulia Trust leo
wilayani Tukuyu mkoani Mbeya. Wa kwanza kushoto ni Mwasisi wa taasisi
hiyo ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Tulia Ackson.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala akifungua tamasha la ngoma za jadi leo
wilayani Tukuyu mkoani humo, ambapo amesisitiza Watanzania kukuza na
kuendeleza utamaduni wa Mtanzania hatua inayoongeza fursa ya ajira kwa
vijana mkoani humo.
Naibu
Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson
akipokea zawadi ya CD kutoka kwa Mchungaji Damian Matipa wa Kanisa la
Uponyaji Mbeya mjini yenye nyimbo za kumpongeza Naibu Spika kwa kazi
anazofanya.
Naibu
Spika Dk. Tulia Ackson
akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel mara baada ya kuwasili Tukuyu mkoani
Mbeya.
Naibu
Spika Dk. Tulia Ackson
akiteta jambo na Mkuu wa Majeshi Mtaafu Jenerali Davis Mwamunyange
wakati wa tamasha la ngoma za jadi linaloratibiwa na Taasisi ya Tulia
Trust leo wilayani Tukuyu mkoani Mbeya.
Ngoma ya Bugobo gobo kutoka Bujara mkoani Mwanza
Baadhi
ya viongozi wakiwa wamebeba moja ya vifaa Bugoyangi (nyoka)
vinavyotumiwa na kikundi cha kucheza ngoma cha Bujora mkoani Mwanza.
Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Tukuyu, Mbeya
Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Tukuyu Mbeya
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante
Ole Gabriel amewataka Watanzania kuenzi na kuimarisha utamaduni wao ili
kuepukana na chamgamoto ya utamaduni kutoka nchi za magharibi unaoleta
ukuaji wa sayansi na teknolojia.
Prof.
Elisante ametoa kauli hiyo leo Tukuyu wakati wa ufunguzi wa tamasha la
Ngoma za jadi linaloratibiwa na Taasisi ya Tulia Trust inayoongozwa na
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia
Ackson inayojishughulisha na masuala ya kukuza na kuendeleza utamaduni
nchini.
Prof.
Elisante amewahakikishia vijana kuwa kuwekeza mahali salama, hivyo
waendelee kukuza sanaa yao iweze kujijengea jina na kutambulika ndani na
nje ya nchi.
“Vijana
muendelee kuthamini utamaduni wetu, tusiposimamia, kuwekeza na
kuthamini utamaduni wetu, utamaduni wan chi za magharibi utawachukua
vijana wetu na kuacha tunu yetu ya asili tangu enzi za babu zetu”
alisema Prof. Elisante
Prof.
Elisante amewahakikishia waandaaji wa tamasha hilo kuwa Serikali ipo
sambamba nao na kuwataka wapanue wigo wa tamasha hilo ili liweze kuwa na
matawi na kuwafikia watu wengi zaidi nchi nzima.
Akifungua
tamasha hilo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala amesema limekuwa
kichocheo cha kukuza na kuendeleza utamaduni wa Mtanzania hatua
inayoongeza fursa ya ajira kwa vijana mkoani Mbeya.
“Utamaduni
ukitumika vizuri una fursa nyingi kwa vijana katika maeneo mbalimbali
ikiwemo tasnia ya sanaa ambayo itawasaidi kujipatia ajira hatua
inayowasaidia kuinua kipato chao na uchumi wa taifa” alisema Mkuu huyo
wa mkoa.
Kwa
upande wake Mwasisi wa Taasisi ya Tulia Trust ambaye pia ni Naibu Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson amesema
kuwa tamasha hilo linafanyika kwa mara ya pili ambapo mwaka huu limakuwa
na wigo mpana kwa kushirikisha vikundi vya ngoma kutoka maeneo
mbalimbali nchini.
Kuhusu
manufaa ya tamasha hilo, Dkt. Tulia amesema kuwa mwaka jana taasisi
hiyo ilipeleka vijana 20 kupata mafunzo ya kitaalamu kwenye fani ya
sanaa na utamaduni katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo
(TaSUBa) na mwaka huu wanatarajia kupeleka vijana 27 ili waweze kupata
ujuzi utakaowasaidia kufanya shughuli zao kwa tija.
Tamasha
hilo linahusisha mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza, Lindi, Katavi,
Dodoma, Kagera, Tanga, Mtwara, Kigoma na wenyeji mkoa wa Mbeya.
No comments