SAMATTA, MSUVA NA BANDA WAZIBEBA TIMU ZAO
![]() |
Mbwana Samatta (katikati), akiiungana na wenzake kumpongeza mfungaji wa bao la jana, Alejandro Pozuelo Melero
|
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Samatta juzi amesaidia timu yake ya KRC Genk kusonga mbele kwenye mchezo wa Kombe la Ubelgiji baada ya ushindi wa ugenini wa bao 1-0 dhidi ya Cercle Brugge uliofanyika kwenye Uwanja wa Jan Breydelstadion mjini Brugge.
NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Samatta juzi amesaidia timu yake ya KRC Genk kusonga mbele kwenye mchezo wa Kombe la Ubelgiji baada ya ushindi wa ugenini wa bao 1-0 dhidi ya Cercle Brugge uliofanyika kwenye Uwanja wa Jan Breydelstadion mjini Brugge.
Bao pekee la Genk lilifungwa na kiungo Mspaniola Alejandro Pozuelo Melero dakika ya 18 na baada ya sare ya 0-0 kwenye mchezo wa kwanza nyumbani, Genk sasa inasonga mbele kwa ushindi wa ugenini.
Samatta jana alicheza dakika 75, kabla ya kumpisha mshambuliaji kinda wa umri wa miaka 21, Mdenmark, Marcus Ingvartsen.
![]() |
Simon Msuva (kushoto) akifurahia na wachezaji wenzake jana nchini Morocco |
Mshambuliaji huyo wa zamani wa African Lyon, zamani Mbagala Market na Simba zote za Dar e Salaam, amefunga mabao 21.
Cercle Brugge ; Van Damme, Taravel, Vincent, Bruno/Barcelos dk57, Omolo, Robail/Buyl dk80, Gaspar, Imorou, De Belder, Mercier/Tormin dk68 na Sofranac.
KRC Genk: Vukovic, Mata, Aidoo, Brabec, Khammas, Heynen, Berge, Pozuelo/Malinovskyi dk75, Benson/Buffalo dk85, Writers na Samatta/Ingvartsen dk75.
Mapema juzi, mchezaji mwingine wa Tanzania anayecheza nje, beki Abdi Banda aliisaidia timu yake ya Baroka FC kushinda mabao 2-0 ugenini dhidi ya wenyeji, Bloemfontein Celtic katika mchezo wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini, mabao ya Sipho Moeti dakika ya 43 na Gift Motupa dakika ya 87.
Mchezaji mwingine wa Tanzania, Simon Msuva, usiku wa juzi aliisaidia timu yake ya Difaa Hassan El-Jadida kusonga mbele katika Kombe la FA Morocco baada ya sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Ittihad Tanger Uwanja wa Grand Stade de Tanger.
Msuva aliyejiunga na timu hiyo Julai mwaka huu akitokea Yanga ya Dar es Salaam, alicheza dakika 90 na alikuwa ana mchango mkubwa uwanjani. Mchezo wa kwanza timu hizo zilitoshana nguvu na juzi Difaa imesonga mbele kwa faida ya bao la ugenini.
kwa hisani ya www.binzubeiry.co.tz
No comments