WATU SABA WAFARIKI KWA AJALI

Picha haihusiani na habari hapa chini
Watu saba wamefariki katika ajali mbili tofauti ambapo ajali ya kwanza
watu wawili wa familia moja wamepoteza maisha na wengine sita kujeruhiwa
katika ajali ya gari dogo aina ya Kluger iliyotokea eneo la Masaki
mkoani Pwani leo.
Majeruhi sita wa ajali ya gari ndogo iliyotokea mkoani Pwani wamelazwa
katika hospitali ya wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani na taratibu
zinafanyika ili kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa
matibabu zaidi kutokana na hali zao kuwa mbaya.
Aidha watu wengine watano wamefariki dunia na wengine zaidi ya 20
kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha lori la mzigo lililokuwa limebeba
abiria mkoani Singida.
Ajali zote mbili zimesababisha vifo vya watu saba huku wengine 26 wakiwa ni majeruhi.
Kwa hisani ya www.malunde.com
No comments