 |
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu
akiwa ameshikilia vifaa vya kuchomelea vyuma kuashiria kuanza kuweka msingi wa
kivuko ‘’Keel Laying’’ katika eneo la Pasiansi ikiwa ni kumbukumbu ya kuanza
rasmi kwa ujenzi wa kivuko kipya kitakachotoa huduma kati ya Kigongo na Busisi
Mkoani Mwanza. Ujenzi wa kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari
2018 na utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 8.9.
|
 |
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu
akichomelea vyuma kuashiria kuweka msingi wa kivuko ‘’Keel Laying’’ katika eneo
la Pasiansi ikiwa ni kumbukumbu ya kuanza rasmi kwa ujenzi wa kivuko kipya
kitakachotoa huduma kati ya Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Ujenzi wa kivuko
hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya
shilingi Bilioni 8.9.
|
 |
Meneja wa Miradi wa Kampuni ya Kizalendo ya MS. Songoro Marine Transport
Limited ya Jijini Mwanza Major Songoro (kushoto) akitoa maelezo kwa Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (kulia) kuhusu
kuanza kwa mradi wa ujenzi wa kivuko kipya cha Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza.
Ujenzi wa kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na
utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 8.9.
|
 |
Meneja wa Miradi wa Kampuni ya Kizalendo ya MS. Songoro Marine Transport
Limited ya Jijini Mwanza Major Songoro (kulia) akimuonyesha Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto) michoro itakayotumika
katika Ujenzi wa kivuko kipya cha Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Ujenzi wa
kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya
shilingi Bilioni 8.9.
|
 |
Meneja wa miradi wa Kampuni ya Kizalendo ya MS. Songoro Marine Transport
Limited ya Jijini Mwanza Major Songoro (kulia) akimuonyesha Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (katikati) michoro itakayotumika
katika Ujenzi wa kivuko kipya cha Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Kushoto ni
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Songoro Bwana Salehe Songoro. Ujenzi wa
kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya
shilingi Bilioni 8.9.
|
 |
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kizalendo ya MS. Songoro Marine Transport
Limited ya Jijini Mwanza Bwana Salehe Songoro (wa pili kulia aliyenyoosha mkono) akimuonyesha
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (wa tatu
kushoto) mojawapo ya malighafi itakayotumika katika ujenzi wa kivuko kipya cha
Kigongo na Busisi. Ujenzi wa kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo
Januari 2018 na utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 8.9.
|
Na Alfred Mgweno (TEMESA MWANZA)
Mtendaji Mkuu
wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu, ameshiriki katika
zoezi la kuweka msingi wa ujenzi wa kivuko kipya kitakachotoa huduma ya usafiri
katika Ziwa Victoria kati ya Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza.
Zoezi hilo linaloashiria kuanza rasmi kwa ujenzi huo limefanyika
Pasiansi katika eneo linalotumika kwa ajili ya ujenzi wa meli, vivuko na boti
linalomilikiwa na Kampuni ya Songoro Marine Transport Limited ya Mwanza
iliyoshinda zabuni ya kujenga kivuko hicho kwa gharama ya sh. bilioni 8.9
za kitanzania.
Tukio hili la kihistoria lilihudhuriwa pia na
Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko kutoka TEMESA Mhandisi
Japhet Maselle, Mhandisi Amos Mutahiwa kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Bwana Salehe Songoro Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Songoro, na
wafanyakazi wa Kampuni ya Songoro na wale wa TEMESA.
Akiongea baada
ya zoezi hilo, Dk. Mgwatu amesema wakazi wa Mwanza wana kila sababu ya
kujivunia kuanza kwa ujenzi wa kivuko hicho kwani kitakapokamilika kitasaidia
kurahisisha usafiri wa abiria na mali zao na hivyo kuimarisha uchumi wao.
Dk. Mgwatu amemtaka Mkandarasi kuhakikisha anamaliza kujenga kivuko ndani ya
muda uliopangwa kwenye mkataba na kuzingatia ubora wa hali ya juu. Pia
ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutenga fedha za maendeleo kwa ajili ya
miradi ya vivuko kwa lengo la kuboresha huduma za usafiri.
Naye Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Songoro ameahidi kukamilisha mradi huo kwa wakati huku
akisisitiza kuwa kampuni yake imejipanga vyema kufanya kazi kwa kasi kwa kuwa
malighafi kwa ajili ya ujenzi wa kivuko tayari ipo kwenye eneo la ujenzi.
Kivuko hicho
kipya kitakapokamilika kitafanya idadi ya vivuko vinavyotoa huduma katika eneo la
Kigongo Busisi kufikia vinne vikiwemo vile vya MV. Sengerema, MV. Misungwi,
pamoja na MV. Sabasaba.
No comments