YANGA YAENDELEA KUJIFUA UWANJA WA UHURU
![]() |
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Burundi Amis Tambwe akiwa katikati akipambana na wachezaji wa Yanga katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. |
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Kikosi
cha Yanga kimeendelea tena na mazoezi mapema leo baada ya kupewa
mapumziko ya siku mbili kutoka kwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Mzambia
George Lwandamina.
Yanga
waliokuwa wanafanya mazoezi ya Gym kwa takribani wiki moja na nusu
ikiwa ni katika programu ya Mwalimu Lwandamina ya kuwaweka fit wachezaji
hao baada ya kuwa mapumzikoni kwa kipindi kirefu.
Leo
mapema asubuhi kikosi hicho kiliingia katika Uwanja wa Uhuru kwa ajili
ya kuendelea na mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu 2017/18
huku wakitarajiwa kuwa mechi kadhaa za kirafiki.
Mechi
ya kwanza ya kirafiki itakuwa ni Agosti 5 dhidi ya timu ya Singida
inayonolewa na aliyewahi kuwa kocha wa timu hiyo Mholanzi Hans Van De
Pluijm mchezo utakapigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.

Beki wa kulia wa Yanga Juma Abdul akiwa amemiliki mpira akijaribu kumtoka mchezaji mwenzake katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.

Wachezaji wa Yanga wakiwa katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.

Kocha
George Lwandamina akijadiliana jambo na Beki kisiki Kelvin Yondani
katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini
Dar es salaam.
No comments