WAZIRI LUKUVI AMSIMAMISHA MUWEKEZAJI WA MKONGE MKOANI TANGA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na wakazi wa kata ya
Mnazi wilaya ya Lushoto mkoni Tanga waliozuia msafara wake na kumpa
malalamiko kuhusu mashamba matatu yaliyotelekezwa na mmiliki wa mashamba
hayo bila kuendelezwa na kusababisha migogoro.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akikagua mashamba ya katani
yanayomilikiwa na kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited yaliyopo kata
ya Mnazi wilayani Lushoto mkoani Tanga.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akikagua miundombinu na
mazingira ya kazi ya mwekezaji wa kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited
ambaye ameshindwa kuindeleza tangu akabidhiwe mwaka 1997.

Mazingira ya shamba
yaliyotelekezwa na mmiliki wake wa kampuni ya Le-Mash Enterprises
Limited ambaye ameshindwa kuindeleza tangu akabidhiwe mwaka 1997.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na Kamishna wa Ardhi
Kanda ya Kaskazini Bwana Leo Komba kuhusu hatua zilizochukuliwa na ofisi
yake hadi sasa kwa mmiliki ambae ameshindwa kuwa na sifa za umiliki na
hajalipa kodi ya ardhi tangu mwaka 2004

Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na wakazi wa kata ya
Mnazi wilayani Lushoto mkoani Tanga kuhusu shamba hilo linalostahili
kufutwa kama ilivyopendekezwa na ofisi ya Mkoa wa Tanga na ofisi ya
Kamishna wa Ardhi Kanda ya Kaskazini kwa kuwa mmiliki.

Baadhi ya mitambo iliyochakaa
ambayo mwekezaji wa kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited ameshindwa
kuiendeleza tangu akabidhiwe mwaka 1997 kwa kurithi mashine na mitambo
hiyo kutoka kwa mkoloni tangu mwaka 1937.

Baadhi ya mitambo iliyochakaa
ambayo mwekezaji wa kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited ameshindwa
kuiendeleza tangu akabidhiwe mwaka 1997 kwa kurithi mashine na mitambo
hiyo kutoka kwa mkoloni tangu mwaka 1937.
……………………………………………………………………………..
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesimamisha umiliki wa
mwekezaji wa mashamba ya katani yanayomilikiwa na kampuni ya Le-Mash
Enterprises Limited yaliyopo kata ya Mnazi wilayani Lushoto mkoani
Tanga.
Waziri Lukuvi amefikia uamuzi huo
baada ya wakazi wa eneo hilo kuzuia msafara wake na kupata malalamiko
mengi kutoka kwa wananchi hao na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya
Lushoto wakimlalamikia Waziri kuhusu mashamba matatu ya Mnazi
yaliyotelekezwa na mmiliki wa mashamba hayo bila kuendelezwa na
kusababisha migogoro kwa awakazi wa Mnazi.
Baada ya kupokea malalamiko hao
Waziri Lukuvi aliamua kutembelea mashamba hayo na kuyakagua ili kujionea
hali halisi na kuwasikiliza wananchi ambao wamekuwa wanakabiliwa na
mgogoro huu kwa miaka mingi.
Baada ya kutembelea na
kujiridhisha Waziri Lukuvi amesema kwamba shamba hilo linastahili
kufutwa kama ilivyopendekezwa na ofisi ya Mkoa wa Tanga na ofisi ya
Kamishna wa Ardhi Kanda ya Kaskazini kwa kuwa mmiliki ameshindwa kuwa na
sifa za umiliki kwa kuwa hajalipa kodi ya ardhi tangu mwaka 2004,
hajalipa wafanyakazi wake kwa muda mrefu, miundombinu yake na mazingira
ya kazi hayaridhishi na ameshindwa kuliendeleza shamba hilo tangu
akabidhiwe mwaka 1997 kwa kurithi mashine na mitambo ileile ya mkoloni
ya mwaka 1937.
Aidha, katika ziara hii Waziri
Lukuvi amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela na Mkuu wa
Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera ili kutatua migogoro ya mipaka iliopo
kati ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara na Wilaya ya Kilindi mkoani
Tanga ikiwa ni muendelezo wa mikutano ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro huu
ambao umesababisha uvunjifu wa amani.
Waziri Lukuvi anatekeleza agizo
la Waziri Mkuu Mhe. Khassim Majaliwa ambae alimuagiza Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kutatua mgogoro huu
uliodumu kwa miaka mingi kati ya Wilaya hizo mbili pindi alipofanya
ziara yake mkoani Tanga.
Mnamo tarehe 18 Januari, 2017
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifanya ziara Wilayani Kilindi katika
Kijiji cha Mafisa na kuzungumza na wanachi Kijijini hapo kuhusiana na
mgogoro huo na kutoa maagizo kwa viongozi wa kuchaguliwa kuacha kutumia
nafasi zao vibaya kuongoza kwa mihemko au ushabiki kwa kuwa kufanya
hivyo kunapelekea wananchi kufuata ushabiki na kuvunja sheria zilizopo.
Ili kutekeleza agizo hili wakuu
wa mikoa hii miwili wakiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Mhe. William Lukuvi wamekutana ikiwa ni muendelezo wa vikao
vya kulitafutia ufumbuzi suala hili.
No comments