![]() |
Wilson Makubi |
DAR ES
SALAAM FILM ACADEMY – D.F.A
Dar es Salaam Film Academy (D.F.A), ni taasisi ya
mafunzo sanaa kwa mafunzo ya tasnia filamu, kwa kushirikiana na wataalamu
mbalimbali nchini, D.F.A Itaanza kutoa mafunzo ya taaluma za utayarishaji wa filamu, Uongozaji wa michezo
ya filamu na tamthilia, Uandishi wa Miswaada ya filamu, Uhariri wa kazi za
filamu na maigizo, n.k.
D.F.A baada ya kufanya tafiti nyngi kuhusu kushuka
kwa tasnia ya Filamu Tanzania, pamoja na kwamba Serikali imeanza kurasimisha
shughuli za Wasanii hasa wa Filamu na Muziki. Lengo la Serikaili lilikuwa jema
katika kuleta heshima na kuboresha uchumi wa Wasanii ikiwemo na kutambua
mchango wa tasnia za Sanaa katika pato la Taifa.
Kutokana na Utafiti huo
D.F.A imegundua kwamba filamu za Wasanii wa Tanzania zimekosa soko kwa Sababu
nyingi zikiwemo zifuatazo
1.
Viwango duni vya Wasanii
wengi wa Filamu Tanzania
2.
Kutokuw na Weledi (Elimu)
wa Kitaaluma kwa Waongozaji wengi ambao wameonekana kutokuwa Wabunifu wakati
teknolojia ikisonga mbele kwa kasi wao wako ktik fikra zile za kizamani
3.
Waandishi na Watunzi wengi
kurudia namna na hadithi zilizoandikwa na kuchezwa na Wasanii waliopita.
4.
Ubinafsi uliokithiri kwa
baadhi ya Wasanii waliotangulia
5.
Serikali kutozitazama
tasnia za Sanaa kama ni sehemu ya pato
la Taifa au kuwa ni sehemu ya ajira kwa Vijana wengi ili kuipa vipaumbele vya
mahitaji
Kwa
ufupi tatizo la Elimu ya Taaluma za Uigizaji, Uongozaji na Uandishi wa Script
ni tatizo la Ubora wa kazi za Filamu na Tamthilia Tanzania
D.F.A
imefikia uamuzi wa kuondoa changamoto hiyo na nyinginezo kwa kuandaa kozi
za mafunzo yafuatayo;
1.
Uigizaji (ACTING) wa filamu na Tamthilia
2.
Uongozaji (DIRECTING) wa Filamu na
Tamthilia
3.
Uandishi wa Miswaada (SCRIPT WRITING)
kwa Filamu na Tamthilia
4.
Mbinu Bora za Usambazaji wa Filamu zetu na
Utafutaji wa Mitaji na
Masoko ya nje ya filamu zetu
5.Lugha
ya Kiingereza
6.Sheria
za Hakimiliki na Hakishiriki
Lengo Kuu la Kozi/Program hiyo ni kuwawezesha
Wasanii kuwa na Weledi wa kazi zao ili Kuboresha Filamu zao na kuleta matokeo
Bora.
Mafunzo
yanatarajiwa kuanza 1/9/2017 anayehitaji afike ofisi za Dar es Salaam Film
Academy, Legho Hotel Shekilango Road Sinza.
Kozi
hizo zitaendeshwa kwa muda wa miezi mitatu na Wakufunzi Waliobobea kutoka
TASUBA na University DSM
AHSNTE
NAKUSHUKURU NAOMBA USHIRIKIANO
WILSON
R. MAKUBI
MKURUGENZI
D.F.A
0679
039 888, 0744 668 030
No comments:
Post a Comment