Header Ads

ad

Breaking News

Taasisi kutoa mafunzo ya tasnia ya filamu

Wilson Makubi

              DAR  ES  SALAAM FILM  ACADEMY – D.F.A



Dar  es Salaam Film Academy (D.F.A), ni taasisi ya mafunzo sanaa kwa mafunzo ya tasnia filamu, kwa kushirikiana na wataalamu mbalimbali nchini, D.F.A Itaanza kutoa mafunzo ya taaluma za  utayarishaji wa filamu, Uongozaji wa michezo ya filamu na tamthilia, Uandishi wa Miswaada ya filamu, Uhariri wa kazi za filamu na maigizo, n.k.


D.F.A  baada ya kufanya tafiti nyngi kuhusu kushuka kwa tasnia ya Filamu Tanzania, pamoja na kwamba Serikali imeanza kurasimisha shughuli za Wasanii hasa wa Filamu na Muziki. Lengo la Serikaili lilikuwa jema katika kuleta heshima na kuboresha uchumi wa Wasanii ikiwemo na kutambua mchango wa tasnia za Sanaa katika pato la Taifa.

Kutokana na Utafiti huo D.F.A imegundua kwamba filamu za Wasanii wa Tanzania zimekosa soko kwa Sababu nyingi zikiwemo zifuatazo
1.   Viwango duni vya Wasanii wengi wa Filamu Tanzania
2.   Kutokuw na Weledi (Elimu) wa Kitaaluma kwa Waongozaji wengi ambao wameonekana kutokuwa Wabunifu wakati teknolojia ikisonga mbele kwa kasi wao wako ktik fikra zile za kizamani
3.   Waandishi na Watunzi wengi kurudia namna na hadithi zilizoandikwa na kuchezwa na Wasanii waliopita.
4.   Ubinafsi uliokithiri kwa baadhi ya Wasanii waliotangulia
5.   Serikali kutozitazama tasnia za Sanaa kama  ni sehemu ya pato la Taifa au kuwa ni sehemu ya ajira kwa Vijana wengi ili kuipa vipaumbele vya mahitaji

Kwa ufupi tatizo la Elimu ya Taaluma za Uigizaji, Uongozaji na Uandishi wa Script ni tatizo la Ubora wa kazi za Filamu na Tamthilia Tanzania


D.F.A imefikia uamuzi wa kuondoa changamoto hiyo na nyinginezo kwa kuandaa kozi za  mafunzo yafuatayo;
1. Uigizaji (ACTING) wa filamu na Tamthilia
2. Uongozaji (DIRECTING) wa  Filamu na Tamthilia
3. Uandishi wa Miswaada (SCRIPT WRITING)  kwa Filamu na Tamthilia
4. Mbinu Bora za Usambazaji wa Filamu zetu na  Utafutaji wa Mitaji na
    Masoko ya nje ya filamu zetu
5.Lugha ya Kiingereza
6.Sheria za Hakimiliki na Hakishiriki

Lengo  Kuu la Kozi/Program hiyo ni kuwawezesha Wasanii kuwa na Weledi wa kazi zao ili Kuboresha Filamu zao na kuleta matokeo Bora.
Mafunzo yanatarajiwa kuanza 1/9/2017 anayehitaji afike ofisi za Dar es Salaam Film Academy, Legho Hotel Shekilango Road Sinza.

Kozi hizo zitaendeshwa kwa muda wa miezi mitatu na Wakufunzi Waliobobea kutoka TASUBA na University DSM 

AHSNTE NAKUSHUKURU NAOMBA USHIRIKIANO

WILSON R. MAKUBI
MKURUGENZI
D.F.A
0679 039 888,  0744 668 030

No comments