![]() |
Madonna na Tupac Shakur kulia. ( Getty Images) |
Jaji mmoja nchini
Marekani amesitisha mnada wa vitu binafsi vya mwanamuziki Madonna baada
ya kusema kuwa haki yake ya faragha ilikiukwa.
Chupi ya Madonna, kitabu cha hundi , kichana , picha na barua ya uhusiano kati ya msanii huyo na aliyekuwa mwanamuziki Tupac Shakur ni miongoni mwa vitu vilivyosimamishwa kupigwa mnada.
Madonna anasema kuwa vitu hivyo viliibwa na rafikiye wa zamani.
Barua hiyo ya Tupac ambapo Tupac anasema kuwa uhusiano wake na Madonna ulivunjika kutokana na ubaguzi wa rangi ilitarajiwa kuuzwa kwa dola 400,000.
Wasanii wote wawili walikuwa maarufu sana wakati huo.
No comments:
Post a Comment