DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA MOYO KUTOKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) PEDRO PALLANGYO ASHINDA TUZO YA WATAFITI VIJANA WA KIAFRIKA KWA MWAKA 2017

NA JKCI, DAR ES SALAAM
TAASISI ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) inafuraha kuutaarifu Umma kuwa Daktari wake Bingwa wa
Magonjwa ya Moyo ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Utafiti na Mafunzo Dkt.Pedro
Kisali Pallangyo(pichani), ameshinda tuzo ya watafiti
vijana wa Kiafrika kwa mwaka 2017 (Young African Researchers Awards
2017). Tuzo hiyo imetolewa na Taasisi ya Sayansi na Utafiti ya nchini Misri.
Dkt. Pallangyo alishinda tuzo
hiyo baada ya kufanya utafiti wa kisayansi katika masuala ya
Afya na dawa za binadamu kwa kuandika machapisho 16 katika majarida (Journal)
saba ya Kimataifa ya Afya ya nchini Marekani.
Licha ya kukabidhiwa tuzo
hiyo mshindi huyo atapewa zawadi ya dola za kimarekani 15,000
(zaidi ya milioni 30 za kitanzania), ngao na cheti.
Tuzo hiyo itakabidhiwa mwezi
wa nane mwaka huu mjini Cairo na Rais wa Misri Mhe. Abdi El- Fattah Al-Sis.
Tangu kuanza kutolewa kwa
tuzo ya watafiti vijana wa Kiafrika mwaka 2014 Dkt. Pallangyo ni
mtanzania wa kwanza kushinda. Mshindi wa mwaka jana alitoka nchini Ghana.
No comments