 |
Beki
wa Yanga, Juma Abdul, (kulia) akiruka kuwania mpira na beki wa AFC Leopards
Abwao Marcus, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super
Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, jana Juni 8, 2017.
Picha zote kwa hisani ya Montage Ltd |
MABINGWA
wa soka Tanzania Bara, Yanga, leo imeaga michuano ya SportsPesa Super Cup, kwa
mikwaju ya penalty baada ya kutoka suluhu katika muda wa kawaida wa dakika 90,
kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kwa
matokeo hayo, Yanga wanaungana na watani wao wa jadi Simba, walioondoshwa na
Nakuru All Stars, pia kwa njia hiyo hiyo ya mikwaju ya penalti.
Yanga
imeondoshwa kwa penalty 4-2 dhidi ya mabingwa wa Kenya, AFC Leopards, huku
wachezaji Said Mussa na Said Makapu wakishindwa kukwamisha wavuni mipira yao,
lakini nahodha wa timu hiyo, nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Obrey Chirwa,
wakizitikisa nyavu za wapinzani wao.
Kwa
ushindi huo wa Leopards, ni dhahiri fainali itawakutanisha wakenya, hivyo timu
mojawapo kupata nafasi ya kucheza na Everton ya England inayoshiriki Ligi Kuu.
 |
Mshambuliaji
wa Yanga Obrey Chirwa, akijiandaa kupiga shuti huku akizongwa na mabeki wa AFC
Leopards, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup,
uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, jana Juni 8, 2017 |
 |
Mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadhi
(kulia) akimtoka mpira na beki wa AFC Leopards, Abdallah Salim, wakati wa
mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye
Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, jana Juni 8, 2017.
|
 |
Winga
wa Yanga, Yusuph Mhilu (kushoto) akimfinya beki wa AFC Leopards, Abwao Marcus,
wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa
kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, jana Juni 8, 2017 |
No comments