Rais amteuwa Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro
![]() |
Anna Elisha Mghwira |
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Ikulu,
Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 03 Juni, 2017
amemteua Bibi Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Bibi Anna Elisha
Mghwira anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Saidi Meck Sadiki aliyekuwa
Mkuu wa Mkoa huo.
Wakati
huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Meja Jenerali
Issah Suleiman Nassor kuwa Balozi.
Kabla ya uteuzi
huo Meja Jenerali Issah Suleiman Nassor alikuwa Mkuu wa Operesheni na Mafunzo
wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Halikadhalika,
Mhe. Rais Magufuli amemteua DIGP Abdulrahman Omari Juma Kaniki kuwa Balozi.
Kabla ya uteuzi
huo DIGP Abdulrahman Omari Juma Kaniki alikuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi.
Tarehe ya
kuapishwa kwa wateule wote itatangazwa baadaye.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa
Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
03 Juni, 2017
No comments