Ndege ya Burma iliyo na abiria 100 yatoweka
![]() |
Ramani ya Myanmar ama Burma |
Ndege moja ya jeshi la Burma, iliyokuwa imewabeba zaidi ya watu 100, imetoweka angani.
Hayo ni kwa mjibu wa taarifa kutoka kwa wakuu wa nchi hiyo.
Ndege
hiyo ya kijeshi, ilikuwa ikipaa kati ya Yangon (Rangoon) na mji ulioko
kusini mwa nchi hiyo wa Myeik. Shughuli za kutafuta na kuokoa manusura
zinaendelea.
"Tulipoteza mawasiliano na ndege hiyo mwendo wa saa
nne na dakika 35 leo asubuhi saa za Afrika Mashariki [07:05 GMT], pale
ndege hiyo ilipofika maili 20 magharibi mwa mji wa Dawei," jeshi la
Burma limesema kwa njia ya taarifa.
Kulikuwa wana abiria 105 na wafanyikazi 11 kwenye ndege hiyo, duru kutoka uwanja wa ndege zimeiambia shirika la habari la AFP.
Aidha, jeshi la nchi hiyo halijasema ni watu wangapi walikuwa ndani ya ndege hiyo ya mizigo iliyoundiwa China.
Ndege
za wanajeshi pamoja na helikopta zimetumwa katika eneo hilo katika
shughuli za kuwatafuta manusura au mabaki ya ndege hiyo ambayo kufikia
sasa inaaminika kuwa imeanguka.
Taarifa inaongeza kuwa, ndege hiyo ilikuwa angani ikivuka bahari ya Andaman, pale ilipotoweka.
No comments