MFUNGWA ALIYEHUKUMIWA JELA MIAKA 63 KWA KUBAKA MZUNGU APIGWA RISASI NA POLISI KWENYE MAKALIO

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Julius Mjengi akifafanua jambo
wakati akitoa taarifa ya mfungwa aliyepigwa risasi wakati akitoroka
mahakamani baada ya kufungwa miaka 63 kwa makosa matatu likiwemo kumpaka
binti raia wa kijerumani ,kumfanyia unyang’anyi wa kutumia silaha na
kumpora simu aina ya Iphone 4
………………………………………………………………………………………………
Na MatukiodaimaBlog
MFUNGWA aliyehukumiwa miaka 63 jela kwa kosa la kumbaka binti mmoja raia wa Kijerumani Gangilonga mjini Iringa Rashid Salufu (23), amejeruhiwa kwa kupigwa risasi za miguuni na makalioni wakati akijaribu kuwakimbia polisi kukwepa kutumikia kifungo hicho jela.
Imeelezwa kuwa mfungwa huyo mara baada ya kusomewa hukumu yake na
katika mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi mkoa wa Iringa alipinga adhabu
hiyo mbele ya hakimu kuwa hataweza kutumikia kifungu hicho kwa madai ni
miaka mingi sana.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Julius Mjengi alimweleza
mwandishi wa matukiodaimaBlog leo ofisini kwake kuwa tukio hilo
lilitokea Mei 30 majira ya saa 5 asubuhi mwaka huu katika viwanja vya
makakama ya mkoa wa Iringa jengo la mahakama kuu eneo la Gangilonga
mjini Iringa .
Alisema kuwa mfungwa huyo Salufi ambae ni mkazi wa Flerimo katika
Manispaa ya Iringa alikuwa na kesi CC namba 20/2017 ya kumbaka binti
huyo wa kijerumani (jina limehifadhiwa) mkazi wa Gangilonga Januari 19
mwaka huu wakati binti huyo akielekea nyumbani kwake Gangilonga na baada
ya ubakaji huyo alimnyang’anya simu yake na kumtishia maisha kisha
kumpora simu yake aina ya Iphone 4
Hivyo, alisema kijana huyo alikamatwa akiwa na simu hiyo na kukiri
kosa la kubaka na unyang’anyi wa kutumia silaha na kumjeruhi binti huyo
hivyo kufikishwa mahakamani kwa makosa matatu, mahakama hiyo
ilimhukumu kifungo cha miaka 30 kwa kosa la ubakaji ,miaka 30 kosa la unyang’anyi wa
kutumia silaha na kosa la miaka 3 la uporaji wa simu hivyo kutumikia miaka 63 kwa pamoja .
” Huyu mshitakiwa baada ya kusomewa hukumu alimweleza hakimu kuwa
hawezi kabisa kutumikia miaka hiyo 63 aliyohukumiwa, wakati akitolewa
katika chumba cha mahakama kupelekwa mahabusu ya muda mahakamani hapo
kabla ya kuanza kutumikia adhabu yake alijaribu kutoroka kwa
kujichanganya na wananchi waliofika mahakamani hapo na kutaka kukimbia
kabla ya polisi kufyatua risasi hewani kwa ajili ya kumtaka ajisalimishe
mwenyewe ila hakuweza kufanya hivyo na kutaka kuendelea kukimbia.”
Alisema kamanda Mjengi kuwa kutokana na mfungwa huyo kuendelea kukimbia ndipo askari mmoja aliweza kuifanya kazi hiyo kwa umakini na kufanikiwa kumpiga risasi katika makalio na mguuni na kufanikiwa kumkamata na kumpeleka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa kwa matibabu.
Alisema kamanda Mjengi kuwa kutokana na mfungwa huyo kuendelea kukimbia ndipo askari mmoja aliweza kuifanya kazi hiyo kwa umakini na kufanikiwa kumpiga risasi katika makalio na mguuni na kufanikiwa kumkamata na kumpeleka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa kwa matibabu.
” Nampongeza sana askari aliyefanikisha kumkamata mfungwa huyo kwani
bila umakini wake, polisi tungelaumiwa kuwa, tumemtorosha
mfungwa huyo aliyefungwa miaka 63 kwa ubakaji. Raia wa kigeni waliofika
mahakamani hapo walikuwa wengi sana kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo.”
Mganga wa mifupa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Charles
Lema alisema kuwa hali ya majeruhi huyo inaendelea vizuri na kuwa
atakuwepo wodini kwa wiki zisizopungua 6 akipatiwa matibabu ya majeraha
hayo kwani alisema alijeruhiwa paja la kushoto na mkoano wa kulia .
Alisema hali ya mkono ni nzuri kwani hakuna mfupa ulioguswa na risasi
hiyo ila mguu wake wa kushoto kuna mfupa ulipata majeraha na risasi
moja ilimpata jirani na maeneo yake ya siri .
No comments