KIONGOZI MBIO ZA MWENGE KITAIFA ATAKA KIBITI IDUMISHE AMANI

Mwamvua Mwinyi, Kibiti
KIONGOZI wa mbio za
mwenge kitaifa ,Amor Hamad ,amewaasa wananchi wa Kibiti -Pwani
,kupendana na kuachana na vitendo vinavyoondosha amani ili kuendelea
kufanyakazi zao za kimaendeleo na kiuchumi.
Aidha amewataka
walimu katika shule mbalimbali wilayani hapo,kuhubiri amani na uzalendo
kwa wanafunzi ili waweze kuwa mabalozi ndani ya jamii .
Amesema endapo wanafunzi wataweza kutambua umuhimu wa amani na utulivu wataifikisha majumbani na hatimae kurejesha utulivu .
Amor aliyasema hayo
,wakati akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mjawa na
baadhi ya wananchi mara baada ya kuzindua jengo la nyumba za walimu
sita.
Alisema uchumi katika eneo lolote huinuka kama wananchi wake wanashirikiana kwa umoja.
“Amani ikidumishwa kila mwananchi atatekeleza majukumu yake kikamilifu ,bila hofu yoyote ” alieleza kiongozi huyo .
Amor alieleza
kwamba,zipo baadhi ya nchi ikiwemo Syria ,Sudan ,Congo ambazo zilipitiwa
na ukosefu wa amani suala lililosababisha kudidimia kwa maendeleo .
Alieleza, kutokana na hilo, haina budi kukemea vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani na utulivu kwenye maeneo yetu .
Pia alimuagiza mkuu
wa wilaya ya Kibiti ,Gulam Kifu kusimamia changamoto za ukosefu wa
maabara ,viti vya walimu na jengo la utawala katika shule ya sekondari
Mjawa ,”kero ambazo ziliwasilishwa kupitia ujumbe wa mabango waliokuwa
wamebeba wanafunzi”.
Amor alikemea suala la utoaji rushwa ,matumizi ya madawa ya kulevya na kudai madawa hayo yanapoteza nguvu kazi ya taifa.
Hakusita kuzungumzia mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria na ukimwi ,ili kulinda afya za watu .
Awali akipokea
mwenge wa Uhuru kutoka Mafia , mkuu wa wilaya ya Kibiti ,Gulam Kifu
,alisema mwenge wa Uhuru ,ulitembelea miradi saba iliyogharimu bil
2.288.9.
Kifu ,alieleza kuwa
,kati ya fedha hizo ,nguvu za wananchi wamechangia bil.2.122
,halmashauri sh .mil .3.5 na serikali kuu mil.37.4 .
Akizungumzia masuala
ya kiusalama aliwatoa hofu wananchi na kuwaomba waendelee na shughuli
zao kwani ulinzi upo wa kutosha wa askari Polisi na jeshi .
June mosi mwenge huo
mwaka huu,ulianza mbio zake mkoani Pwani ,kwa kutembelea miradi saba
wilaya ya Mafia ,iliyogharimu zaidi ya sh.bil 36.2,June 3 utakuwa Rufiji
.
Jumla ya miradi 81 yenye thamani ya sh .bil 225.1 mkoani humo, itapitiwa na mbio za mwenge katika wilaya saba .
No comments