BULEMBO APOKEWA KWA KISHINDO WILAYANI BUHIGWE MKOANI KIGOMA

Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Juuia ya WazaziTanzania, Alhaj
Abdallah Bulembo akikabidhiwa chombo cha kiasili cha kuhifadhia chakula
'Hotpot' cha asili ya Kabila la Waha, alipopokewa kwenye Ofisi ya CCM,
Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, jana, kuendelea na ziara yake ya Kichama
mikoani. Anayemkabidhi ni Dynes Wiston. Watatu kushoto ni Mwenyekiti wa
CCM mkoa wa Kigoma Dk. Amani Kabourou.

Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj
Abdallah Bulembo akifurahia zawadi ya 'Hotpot' baada ya kukabidhiwa na
Umoja wa Vijana wa CCM, alipowasili kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya
Buhigwe, mkoani Kigoma, leo, kuendelea na ziara yake ya Kichama mikoani.

Kijana
wa Umoja wa Vijana wa CCM, Agatha Leon, akimvisha skafu, Mjumbe wa
Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya WazaziTanzania, Alhaj
Abdallah Bulembo alipowasili Ofisi ya CCM Wilaya ya Buhigwe mkoani
Kigoma, jana.

Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah
Bulembo akienda Ofisini katika Ofisi ya CCM,Wilaya ya Buhigwe mkoani
Kigoma, jana.

Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj
Abdallah Bulembo akiwasalimia baadhi ya viongozi kabla ya kuingia
ofisini, katika Ofisi ya CCM wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma jana.

Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj
Abdallah Bulembo (kushoto) akiwaunga mkono kuselebuka, wana CCM
waliokuwa wakijimwayamwaya kwa nyimbo za mapokezi, alipowasili kwenye
Ofisi ya CCM Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, jana.

Wana
CCM wakihanikiza shamrashamra nje ya Ofisi ya CCM Wilaya ya Buhigwe
mkoani Kigoma, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya
Wazazi Tanzania Ahaj Abdallah Bulembo alipowasili kwenye Ofisi hiyo, jana.


Mbunge wa Viti Maalum Josephine Ngezabuke, akishiriki
kuselebuka na wana CCM waliokuwa wakijimwayamwaya kwa nyimbo za
mapokezi ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa CCM, Alhaj
Abdallah Bulembo kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, jana.

Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj
Abdallah Bulembo akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM wilaya
ya Buhigwe mkoani Kigoma, leo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo
Elisha Bagwanya.

Katibu
wa CCM Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma Agnes Ndoriki akisoma taarifa
kwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania
Alhaj Abdallah Bulembo.

Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Elisha Bagwanya akimkaribisha
Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania
Alhaj Abdallah Bulembo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dk.
Aman Kabourou.

Wana
CCM wakishangilia wakati Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa
Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo alipokuwa akiwasili
ukumbini kuendesha kikao cha ndani na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
Wilaya ya Buhigwe, Mabalozi, Watendaji wa Chama na wa Serikali, jana.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo akiwasili ukumbini

Wazee wa Chama wa Buhigwe, walioalikwa kwenye kikao hicho wakishangilia

Wana CCM wakitoa burudani ya wimbo kabla ya kikao kuanza

Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj
Abdallah Bulembo akiwatuza wana-CCM hao kwa burudani yao nzuri ya wimbo.

Wajumbe wakinyoosha mikono kuunga mkono jambo

Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah
Bulembo akimpongeza mmoja wa wanachama wapya wa CCM, waliojiunga wakati
wa kikao hicho.

Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj
Abdallah Bulembo akishirikiana na Mwenyekiti wa Wazee wa Kabila la Waha,
Eliakim Balunguza, kumtawaza Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma,
Kanali Marco Gaguti, kuwa Muha kwa kumvalisha vazi la Mpuzu la kabila
hilo, wakati wa kikao hicho, jana.

Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Kanali Marco Gaguti, akikabidhiwa mkuki kulinda mipaka ya wilaya hiyo

Mkuu
wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma akiwa ameketishwa kwenye kigoda
kukamilisha kutawazwa kwake kuwa Muha, alipata fursa ya
kuzungumzana wajumbe wa kikao hicho.
Mkuu
wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Kanali Marco Gaguti akizungumza
huku akiwa ameketi kwenye kigoda. Katika tukio hilo Mjumbe wa Kamati Kuu ya
CCM na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo na
viongozi wengine wakilazimika kuchuchumaa kwani ni sharti kuwa kila
mtu awe amekaa au amechuchumaa wakati kiongozi wa kabila la Waha mwenye
kuheshimika anapozungumza akiwa amekaa kwenye kigoda.
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi, Alhaj Abdallah
Bulembo akimkabidhi zawadi ya mbuzi Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali
Marco Gaguti, kwa niaba ya wazee wa Buhigwe.
Mwenyekiti
wa Wazee wa Buhigwe Eliakim Balunguza akimkabidhi zawadi ya mbuzi,
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania,
Alhaj Abdallah Bulembo, wakati wa kikao hicho.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Kigoma, Dk. Amani Kaborou akimkaribisha Mjumbe wa Kamati
Kuu ya CCM na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah
Bulembo kuzungumza kwenye Kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
Wilaya ya Buhigwe, mabalozi na watendaji wa chama, jana. Kulia ni
Katibu wa CCM Mkoa wa Kigoma, Naomi Kapambala na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo, Elisha Bagwanya.
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Alhaj
Abdallah Bulembo na meza kuu wakiwa wamesimama baada ya shamrashamra kulipuka ukumbini kabla ya kuanza kuzungumza na wajumbe kwenye kikao
hicho.
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj
Abdallah Bulembo akizungumza na wajumbe kwenye kikao hicho.
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Alhaj Abdallah
Bulembo, akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya
Buhigwe, mabalozi, watendaji wa CCM na wanachama, akiwa katika ziara ya
Kichama mikoani, jana. PICHA: BASHIR NKOROMO
No comments