AFC LEOPARDS YATOCHAPA SINGIDA UNITED KWA PENALTI MECHI ZA PORTPESA SUPER CUP

Singida
United imeng'olewa katika michuano ya SportPesa Super Cup baada ya
kuchapwa kwa mikwaju 5-4 dhidi ya ACF Leopards ya Kenya.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo. Dakika 90 zilimalizika kwa sare ya mabao 1-1.
AFC
Leopards ndiyo waliosawazisha baada ya Singida United inayonolewa na
kocha wa zamani wa Yanga, Hans van der Pluijm kutangulia kufunga bao.
Hata
hivyo, Leopards walionekana kuwa na kasi zaidi hasa katika kipindi cha
pili kwani pamoja na kupata bao la kusawazisha lakini walitengeneza
nafasi nyingi zaidi za kufunga.





No comments