Header Ads

ad

Breaking News

Ziara Maalum ya Rais wa Zanzibar Kisiwani Pemba

Rais wa Zanzibar na Mwenyekikti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati), alipofika katika daraja la Chamanangwe leo kisiwani Pemba lililokatika kutokana na maji ya mvua zilizonyesha hivi karibuni na kusababisha usumbufu kwa wanaotumia daraja hilo kutoka upande mmoja kuelekea sehemu nyengine   wakati alipofanya ziara maalum ya siku moja  ya kikazi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekikti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipofika kijiji cha Gando kumfariji na kumpa pole Mzee Juma Mjaka Khamis (kulia) akiwa na Familia yake aliyepata maafa ya nyumba yake kuangukiwa na mti na kupelekea kukosa sehemu ya kuishi baada ya mvua kubwa za masika zilizonyesha hivi karibuni kisiwani humo


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto), alipokuwa akiangalia jengo la ZSTC Mkoani Pemba lililoanguka ukuta kutokana na kuangukiwa na mti baada ya mvua kubwa za masika zilizonyesha hivi karibuni na kusababisha uharibifu mkubwa alipofanya ziara maalum leo (kushoto) Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe,Amina Salum Ali. (PICHA ZOTE NA IKULU)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekikti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto), alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, Hemed Suleiman alipotembelea Kijiji cha Makombeni wilaya hiyo kuangalia  nyumba mbalimbali za wananchi zilizopatwa na athari  zilizotokana na mvua zinazoendelea kunyesha kisiwani humo leo wakati alipofanya ziara maalum ya kikazi.

No comments