Mkuu wa Mkoa Shinyanga afanya ziara wilayani Kishapu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza na
ujumbe alioambatana nao akiwa katika shamba la mtama kijiji cha Busongo kata ya
Mwamashele. Wengine pichani katikati ni Mkuu wa wilaya hiyo, Nyabaganga Taraba
na Ofisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika, George Kessy.
Mwandishi Wetu, Kishapu
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack amefanya ziara
katika wilaya ya Kishapu na kutembelea na kukagua maeneo yenye fursa mbalimbali
za uwekezaji viwanda.
Katika ziara hiyo Telack aliweza kutembelea vikundi vya
wananchi wanaotengeneza bidhaa za ngozi, mbunifu wa mashine za kukoboa nafaka
na wakulima wa zao la mtama kata ya Mwamashele.
Akiwa katika kata ya Kishapu eneo la Mhunze alitembelea
wanakikundi cha Badimi na kujionea bidhaa mbalimbali za ngozi zikiwemo viatu kuwataka
Watanzania kupenda bidhaa za nchini.
Akiwa ameambatana na mwenyeji wake Mkuu wa wilaya hiyo,
Nyabaganga Taraba pamoja na viongozi mbalimbali alisifu jitiada za kikundi
hicho huku akiwataka Watanzania kupenda bidhaa za ndani.
Kwa upande wao vijana hao walimhakikishia kuwa wanaweza
kutengeneza viatu kw ajili ya mkoa mzima lakini wanakabiliwa na changamoto ya
uhaba wa malighafi na mashine.
Mkuu wa wilaya, Taraba alisema halmashauri hiyo iko nao
bega kwa bega na tayari imetenga fedha kiasi cha sh. milioni 18 katika mwaka
ujao wa fedha ili kukisaidia kikundi hicho.
Katika ziara hiyo pia mkuu huyo wa mkoa alimtembelea mwananchi
Daudi Nkende ambaye mbunifu wa mashine za kukoboa nafaka zikiwemo mtama katika
eneo la Uchunga.
Telack alisema kuwa Serikali imefungua milango kwa
wabunifu wa vitu mbalimbali na hivyo washiriki ili kuunga mkono jitihada zake
katika kutekeleza Sera ya Viwanda.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba
akimuonesha Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack maeneo yaliyotengwa kwa
ajili ya fursa za uwekezaji viwanda eneo la Uchunga. Wengine pichani kulia ni
Katibu Tawala Wilaya, Shadrack Kangese, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri
ya wilaya hiyo, Mang’era Mang’era.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kulia) na
Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba wakiangalia namna mzani wa kupimia
choroko unavyofana kazi katika eneo la Mhunze.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza
ndani ya kiwanda kidogo cha kutengeneza bidhaa za ngozi zikiwemo viatu wakati
wa ziara hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza na
baadhi ya wafanyabishara akiwa katika eneo la Mhunze wakati wa ziara hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akiangalia
viatu vilivyotengenezwa na kikundi cha Badimi wakati wa ziara hiyo.
No comments