WATOTO PACHA WAFANYIWA UPASUAJI KATIKA NJIA MKONO
Daktari
bingwa wa upasuaji wa watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
(MNH, Dk Victor Ngotta (kushoto) akimfanyia upasuaji Eliudi leo kwa
kushirikiana na Profesa Saber Waheeb (katikati) na Dk Mohamed Malak
kutoka Misri (kulia).
Daktari
Bingwa Watoto wa Upasuaji, Dk. Zaituni Bokhary akizungumza jambo baada
ya kumfanyia upasuaji mtoto Elikana aliyekuwa na tatizo la mfumo wa njia
ya mkojo Leo.
Daktari
Bingwa wa Upasuaji, Yona Ringo akiwa ofisini baada ya kumfanyia
upasuaji mtoto Elikana ambaye alikuwa na tatizo la mfumo wa njia ya
mkojo Leo. Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Na John Stephen
Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Leo imefanikisha kuwafanyia upasuaji watoto
pacha ambao walikuwa wana tatizo katika njia mkojo.
Watoto
hao wametoka katika chumba cha upasuaji salama na sasa wanaendelea
vizuri baada ya kurejeshwa wodini. Watoto hao ni Eliudi Joel na Elikana
Joel ambao wana umri wa miaka mitatu kila mmoja.
Daktari
Bingwa Watoto wa Upasuaji, Dk Zaituni Bokhary na Dk Bingwa wa Upasuaji,
Dk Yona Ringo wamefanikisha upasuaji wa Elikana wakati Eliudi
amefanyiwa upasuaji na Profesa Saber Waheeb na Dk Mohamed Malak kutoka
Misri kwa kushirikiana na Dk Victor Ngotta na Dk Mwajabu Mbaga wa
Muhimbili.
Dk
Bokhary amesema kuwa upasuaji wa watoto hao umechukua saa moja na nusu
na kwamba hivi sasa wanaendelea vizuri baada ya shughuli hiyo.
“Watoto hawa wataendelea kuwapo wodini hadi watakapopona vizuri ndio tutawaruhusu,” amesema Dk Bokhary.
Dk Bokhary amesema kuwa watoto wengine wawili leo wamefanyiwa upasuaji ambao walikuwa na tatizo kama hilo.
Jana madaktari wa hospitali hiyo walianza upasuaji kwa watoto wenye matatizo ya njia ya mkojo na mfumo wa hewa na chakul
No comments