Airtel FURSA, VETA YAWAFANIKISHA VIJANA 18,000 KUSOMA UFUNDI STADI KWA SIMU
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel na VETA imeingia mkoani Arusha kuendelea
kutoa uelewa kwa vijana kukamata FURSA na kusomo kozi mbalimbali toka
VETA kupitia mfumo wao wa simu ujulikanao kama VSOMO. hadi sasa zaidi ya
vijana elfu kumi na nane nchini wamejisajili kusoma kwa mfumo huo wa
simu za mkononi huku mikakati yao ikiwa ni kuongeza kozi 10 zaidi ili
wanafunzi kuendelea kujisomea.
Hayo
yamebainishwa na Mkuu wa mauzo kanda ya kaskazini Bw, Brighton
Majwala wakati alipoongea na wajasiliamali na madereva bodaboda
waliokusanyika stand kuu Arusha jana,
“Airtel
na Mamlaka ya ufundi stadi VETA lengo letu ni kuwafikishia elimu ya
ufundi vijana wengi nchini, upande wetu Airtel tunahakiksha mtandao upo
vyema ili vijana waweze kusoma bila kukwama, hadi leo hii tayari vijana
zaidi ya milioni 18 wameshakamata FURSA hii kwa kupakua aplikesheni au
mfumo huu wa VSOMO katika simu zao” alieleza Bw Majwala
Majwala
aliendelea kusema kuwa “mpango wetu Airtel na VETA ni kuongeza uelewa
kwa vijana ili wasome kozi zilizopo sasa ikiwemo ya ufundi piki piki,
umeme wa nyumbani, ufundu simu, ufundi wa aluminium, utaalam wa masuala
ya urembo, pamoja na ufundi wa kuchomea vyuma”.
kwa
upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel alisema “kutokana na VSOMO kuwa
na idadi kubwa ya vijana waliojisajili tayari Airtel kwa kushirikiana
na wadau wetu VETA tuko katika utekelezaji wa kuongeza kozi zingine
zaidi ya kumi ili kuongeza wigo wa kuchagua pamoja na kuongeza idadi ya
wanaosoma na kuhitimu”. alieleza mmbando
“tunampango
wa kuongeza kozi zingine 10 kabla ya mwezi wa 12 ambapo sasa hivi
tayari VETA wako katika utaratibu wa kuzifanyia kazi kozi hizo ili
ziweze kuingia katika mtandao” alisema Mmbando
“Mradi
wa VSOMO ni sehemu ya mpango wa Airtel FURSA wenye lengo la kuwawezesha
vijana pamoja na kutimiza kauli mbiu ya “Airtel the smartphone
network” kwa kujipatia elimu ya ufundi stadi toka VETA kwa smartphone
zao” alisisitiza Mmbando
Airtel
kwa kushirikiana na VETA nchini ilizindua mfumo wa masomo ya ufundi
stadi kwa njia ya mtandao VSOMO mwezi Julai 2016 ambapo mpaka sasa
tayari mfumo huu umetambulishwa katika mikoa ya Dar es salaam, Mbeya,
Arusha, Morogoro na Mwanza lakini kutokana na uhitaji mkubwa kwa vijana
tayari mfumo huo umepokea maombi ya vijana toka mikoa 25 kwa kupakua
mfumo/aplikesheni hiyo hiyo na kuomba kusoma kwa njia ya simu za Airtel.

Meneja
Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando (katikati) akitoa maelekezo kwa
baadhi ya wanaotoa huduma ya usafiri wa Boda boda Arusha eneo la stand
kuu Arusha jinsi wanavyoweza kujiunga na mfumo wa VSOMO na kusoma masomo
ya Ufundi stadi kupitia mtandao wa Airte jana.

Mkuu
wa mauzo wa Airtel kanda ya kaskazini Bw, Bryton Majwala na wafanyakazi
wengine wa Airtel kwa pamoja wakizungumza na baadhi ya wajasiliamali na
watoa huduma ya usafiri wa Boda boda Arusha eneo la stand kuu Arusha
jinsi wanavyoweza kujiunga na mfumo wa VSOMO na kusoma masomo ya Ufundi
stadi kupitia mtandao wa Airtel jana.

Mkuu
wa mauzo wa Airtel kanda ya kaskazini Bw, Bryton Majwala akitoa
maelekezo kwa baadhi ya wajasiliamali wanaotoa huduma ya usafiri wa Boda
boda Arusha eneo la stand kuu Arusha jinsi wanavyoweza kujiunga na
mfumo wa VSOMO na kusoma masomo ya Ufundi stadi kupitia mtandao wa
Airtel mkoani jana.
No comments