Baraza la Ushauri latoa zawadi kwa wanafunzi walioshinda kwenye insha

Kaimu
katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia
sekta Mawasiliano mhandisi Dkt. Maria Sasabo kushoto akizungumza wakati
wa hafla ya kutoa zawadi kwa wanafunzi wa vyuo, sekondari na shule za
msingi za jijini Dar es Salaam walioshinda shindano la uandishi wa insha
kuhusu haki ya mtumiaji wa huduma za mawasiliano, kulia ni Katibu wa
Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano Bi. Mary Shao
Msuya.

Mwenyekiti
wa baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano Bw. Stanley
Mwabulambo akimkaribisha mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi Dkt. Maria
Sasabo kuzungumza na wanafunzi wa vyuo, sekondari na shule za msingi za
jijini Dar es Salaam walioshinda shindano la uandishi wa insha kuhusu
haki ya mtumiaji wa huduma za mawasiliano

Mshindi
wa kwanza wa insha kwa upande wa vyuo vya elimu ya juu Bw. Omari Abbas
kutoka chuo Kikuu kishiriki cha Ualimu (DUCE) akipokea zawadi ya cheti
kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Mawasiliano) mhandisi Dkt. Maria Sasabo.

Mshindi
wa kwanza wa insha kwa upande wa Shule za sekondari Bw, Ramadhani
Mohamed kutoka Shule ya sekondari ya Kibasila akipokea zawadi ya
mshindi wa kwanza wa insha kutoka kwa Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) mhandisi Dkt. Maria
Sasabo.

Mshindi wa kwanza wa insha kwa upande wa Shule za Msingi Jane Michael Andrew kutoka shule ya msingi ya Mbuyuni akipokea zawadi ya cheti ya mshindi wa kwanza wa insha kutoka kwa Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) mhandisi Dkt. Maria Sasabo.
No comments