ACT WAZALENDO WASEMA MCHUANO IRINGA NI CHIKU ,MWAKALEBELA NA MASASI ,MCHUNGAJI MSIGWA ASICHAGULIWE KASHINDWA KAZI
CHAMA
Cha ACT wazalendo kimewataka wananchi wa jimbo la Iringa Mjini kuwapima
wagombea watatu waliojitokeza kuomba kuchaguliwa kupokea nafasi ya
aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Mchungaji Peter Msigwa ( Chadema)kwa
madai kuwa hapaswi tena kupewa kura katika jimbo hilo.
Katibu
Wilaya wa ACT wazalendo Wilaya ya Iringa Bw Zhenepa Ally leo wakati
wa mkutano wa kampeni za Mgombea Ubunge wa jimbo la Iringa mjini Chiku
Abwao ( ACT wazalendo) kwenye kata ya Kitwiru .
Alisema
kuwa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Iringa Mjini Mchungaji Msigwa wakati
wa Ubunge wake awali alikuwa akipambana na ujangili kwa kupambana na
wauwaji wa Tembo na kila mkutano wake alikuwa akionyesha kupiga vita
ujangili ila baada ya kushikamana na Waziri Lazaro Nyalandu ( CCM ) kwa
kusafiri pamoja katika Ziara za nje aligeuka ghafla na kuacha kabisa
kuzungumzia ujangili.
Hivyo
aliwataka wananchi wa jimbo la Iringa Mjini kuwapima wagombea watatu.
Waliojitokeza kuwania nafasi ya Ubunge jimbo hilo ambalo Mchungaji
Msigwa kashindwa kutekeleza ahadi zake kwa wananchi.
Aliwataja
waliojitokeza kugombea nafasi hiyo ya Ubunge ambao wananchi wanapaswa
kuwachuja kuwa ni Chiku Abwao ( ACT wazalendo) ,Frederick
Mwakalebela(CCM) na Daud Masasi (ADC)na sio kupoteza kura kwa kumpa tena
mchungaji Msigwa ambae ametelekeza jimbo hilo kwa miaka yote mitano.
" Katika uchaguzi huu wananchi wa Iringa tunaomba muwapime watu watatu waliojitokeza kumpokea Ubunge Mchungaji Msigwa"
Kwa
upande wake Mgombea Ubunge jimbo hilo la Iringa Mjini Bi Abwao alisema
jimbo la Iringa Mjini ni moja kati ya majimbo ambayo yalikuwa rahisi
zaidi upinzani kuendelea kuongoza tena katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu
ila kutokana na kushindwa kwa Mchungaji Msigwa jimbo hilo wananchi
wamepoteza imani na upinzani.
Abwao aliwaomba wananchi wa jimbo la Iringa mjini kumchague yeye kuwa mbunge wao kwani sera nzuri za kuwakomboa wananchi hao
"
Mbunge Msigwa aliahidi kuwapa nyavu kwa maana ya mitaji ila kipindi
chake chote kaishia kufanya mikutano ya vurugu na kutukana wananchi wake
kuwa ni wavivu wanaopenda kucheza bao wakati nae ni miongoni mwa wavivu
hao na wacheza bao wazuri"
Hivyo
alitaka wananchi wa jimbo la Iringa ili kurejesha heshima ya upinzani
jimbo la Iringa Mjini ni wakati wa kuchagua chama cha ACT wazalendo
kuanzia Udiwani Ubunge na Urais na sio Chadema kupitia mwamvuli wao wa
Ukawa ambao wamesimamisha mgombea ambae yupo katika orodha ya mafisadi.
Akizungumzia
kuhusiana na Mgombea Urais wa Ukawa Chiku ,alisema kuwa Mgombea huyo
hana sifa ya kuwakomboa watanzania kwani ni genge la walanguzi
linalotaka kwenda kutumia Ikulu kwa kurejesha mamilioni ya pesa
waliotumia kununua Ikulu.
Hata
hivyo alisema watanzania wasidanganyike na safari ya matumaini ya Ukawa
kwani safari hiyo haipo tena na hivyo ni vema kuchukua hatua kwa
kukataa wagombea hao wa Ukawa.
No comments