UVCCM WASHAURIWA KUSHAWISHI WENZAO KUKIPA USHINDI CCM
Katibu wa UVCCM Wilaya ya
Mfenesini Haji Machano Juma akisisitiza jambo katika Semina elekezi kwa
Vijana kuelekea Uchaguzi Mkuu iliyofanyika Uroa Kusini Unguja. Kulia
kwake ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Khamis Ali, Mwenyekiti
wa UVCCM Wilaya hiyo Mbarouk Mrakib, na Mlezi wa kundi maalum na Mbunge
wa Vijana Tauhida Galos.
Picha na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Baadhi ya Vijana wa UVCCM kutoka
Wilaya ya Mfenesini wakifuatilia Mada kutoka kwa Viongozi wao hawapo
pichani katika Semina elekezi kwa Vijana hao kuelekea Uchaguzi Mkuu
iliyofanyika Uroa Kusini Unguja.
………………………………………………………
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Vijana wa Chama cha Mapinduzi
UVCCM wamehimizwa kuendelea kuwashawishi WanaCCM wenzao na wale wa Vyama
vya upinzani kuipigia kura CCM ili Chama hicho kiendelee kutawala Bara
na Visiwani.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa
Umoja huo wa Wilaya ya Mfenesini Mbarouk Mrakib wakati akitoa mada
katika Semina elekezi kwa Vijana iliyofanyika Uroa kusini Uguja.
Amesema Vijana ndio watetezi
wakubwa wa Chama nakwamba juhudi zao zinahitajika zaidi kipindi hiki cha
kuelekea Uchaguzi Mkuu ili kukipa ushindi wa kishindo chama hicho
kuliko miaka ya nyuma.
“Tusisahau wajibu wetu ambao ni
kumshawishi kila Mpiga kura bila kujalisha chama chake aipigie kura ya
Ndio CCM kwani ni Chama pekee chenye Nia thabiti ya kuleta mabadiliko ya
Kiuchumi” Alisema Mrakib.
Kwa upande wake Mlezi wa kundi
maalum ambaye pia ni Mbunge wa Viti maalum Tauhida Galos Cassian
amewaomba Vijana wa CCM kuwa na msimamo bila ya kuyumbishwa na Vyama vya
upinzani.
Amesema vyama vyote vinakimbilia
kundi la Vijana kwa vile ndio kundi kubwa na jepesi kushawishika hivyo
kuwasisitiza Vijana hao kuendelea kuiamini CCM ambayo ndio Mkombozi wa
Uchumi.
“CCM imefanya mengi katika Nyanja
mbalimbali ikiwemo Elimu, Uchumi, Miundombinu na Michezo hivyo Wananchi
wanakila sababu ya kuendelea kuiamini ili izidi kuleta maendeleo”Alisema
Tauhida.
Akifungua Mafunzo hayo Mgeni Rasmi
wa Semina hiyo Khamis Ali ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya
Taifa NEC amewataka Vijana hao kushirikiana na kuyatekeleza yale
wanayoambiwa na Viongozi wao.
Naye Katibu wa UVCCM Wilaya ya
Mfenesini Haji Machano Juma amewaomba Vijana walioshiriki Semina elekezi
kuhakikisha Wanatoa elimu kwa Vijana wengine ambao hawakushiriki Semina
hiyo.
Semina hiyo ya kuwajengea uwezo
Vijana hao juu ya mambo mbalimbali yanayohusu Uchaguzi na wajibu wao ili
kufanikisha Ushindi kwa Chama cha Mapinduzi ilifanyika Mwisho wa Wiki
katika Hoteli ya Coconut Uroa Kusini Unguja.
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
No comments