![]() |
Arsenal Wenger |
KOCHA
wa Arsenal, Arsene Wenge, amesisitiza kuwa, hayupo mbali na changamoto za
kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Englanda na Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Katika
taarifa yake, kocha huyo alisema kwamba, baada ya wiki ya kipigo katika mechi ya Kombe
la FA dhidi ya Blackburn, kabla ya kuchapwa mabao 3-1 dhidi ya Bayern Munich kwenye
uwanja wake wa Emirates, aliweka wazi kuwa, kikosi cha Gunners kiko ukingoni
kumaliza ukame wa makombe wa miaka nane.
Hata
hivyo, kocha huyo wa Arsenal, alisisitiza kuwa, ataongeza wachezaji wakali wanaohitajika
katika kikosi chake ambacho kitakuwa cha ushindani chenye mshikamano.
"Hatuko
mbali sana, hata kama ni vigumu kukushawishi leo," alisema Wenger. "Tuna
msingi wa timu ambao ni imara, tunatakiwa kukiimarisha kikosi kwa kuangalia
nafasi za kuzijaza zilizoonesha udhaifu.
"Hatuna
tofauti kubwa na timu kama Bayern, walio katika nafasi kama ilivyo kwa Manchester
United. Wanaweza kumudu kile wanachotaka kukifanya. Wako vizuri kiuchumi. Ukizipeleka
Chelsea na Man City Ujerumani, utasikia tena kuhusu Bayern.
Wenger
aliwataka mashabiki wa Arsenal kuwa wavumilifu, huku akithibitisha kuwa,
anauamini uwezo wake na kikosi chao kitarajea katika makali yao.
No comments:
Post a Comment