“Ninafurahi
kwamba hali ya utulivu imefikia kiwango hiki na nina uhakika FIFA itafanya
uchunguzi wa kina na kufanya uamuzi kwa maslahi ya mpira wa miguu,” amesema
Mamelodi alipokuwa akizungumzia uchaguzi mkuu wa TFF ambao ulikuwa ufanyike
Februari 24 mwaka huu lakini ukasimamishwa kutokana na matatizo kadhaa baada ya
baadhi ya wagombea kuenguliwa.
Mbali
na kuhudhuria Mkutano Mkuu wa TFF na uchaguzi, safari ya Mamelodi nchini pia
ilihusisha kumtambulisha msaidizi wake, Patrick Onyango ambaye amejiunga na
ofisi hiyo ya FIFA kuanzia mwishoni mwa mwaka jana, kufuatilia miradi ya
maendeleo ikiwa ni pamoja na GOAL Project 4 ambayo ni uwekaji wa nyasi bandia
kwenye Uwanja wa Nyamagana na maendeleo ya Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba,
mikakati ya mwaka 2013 na kozi mbalimbali.
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Mikutano wa TFF jana, Mamelodi alisema
uamuzi wa Shirikisho hilo kutuma wajumbe katikati ya mwezi ujao unatokana na
mawasiliano baina ya Rais wa TFF, Leodegar Tenga na FIFA ambayo ilitaarifiwa
hali halisi ilivyo na kama inaweza kusaidia kutatua matatizo yaliyopo.
“FIFA
haitakuja kuingilia mchakato wa uchaguzi, itakuja kutatua matatizo,” amesema
Mamelodi. “Masuala ya uchaguzi ni ya ndani ya nchi. FIFA haiji kuichagulia
Tanzania rais. Wajumbe wanaweza kumchagua mtu yeyote wanayeona kuwa anafaa kuwa
rais,” amesema Mamelodi.
“Lakini
katiba ya FIFA iko wazi kwamba mwanachama wake ni lazima akubaliane na sheria
za Shirikisho kuwa wanachama ni lazima wabanwe na Katiba ya FIFA. Kwa hiyo mara
tu unapopata uanachama wa FIFA, ni lazima ujue kuwa utabanwa na katiba ya FIFA
na mojawapo ya mambo haya.
“Lakini
kuna tofauti na kitendo cha Serikali kusimamisha uchaguzi kwa kuwa hiyo inakuwa
ni Serikali kuingilia moja kwa moja masuala ya mpira wa miguu, kitu ambacho
katiba ya FIFA inakataza.”
Mamelodi,
ambaye alitumia muda mwingi kuelezea umuhimu wa hali ya utulivu iliyotawala kwa
muda mrefu nchini, amesema anajua kuwa uongozi wa Rais wa sasa wa TFF, Leodegar
Tenga umefanya mengi katika kuhakikisha unajenga mazingira mazuri ya maendeleo
ya mpira wa miguu, lakini kuna wakati ni lazima uheshimu uamuzi wa mtu.
“Tenga
amesema imetosha anaondoka na hatuna budi kuheshimu uamuzi wake. Hiyo ni kauli
inayotoka kwa kiongozi wa kweli, kiongozi anayewajibika. Lakini kwa kuangalia
misingi ambayo uongozi wake umeijenga, ni wazi kuwa kiongozi mpya ataendeleza
taasisi bila ya matatizo.
“Tanzania
haikufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika, lakini kuna miradi mingi ya
maendeleo ambayo ilifanyika, mingine ambayo ilijaribiwa kwa mara ya kwanza
nchini Tanzania na ikafanikiwa. Kuna Azimio la Bagamoyo, Semina ya Mawasiliano
ya Jamii (Comm-Unity) ya Wanawake, Futuro III na mingine. Yote hii ilifanyika
kwa sababu kulikuwa na utulivu.
“Hivi
sasa TFF ina sekretarieti ina Mkurugenzi wa Ufundi; ina programu za maendeleo
na kuna utulivu. Cha msingi ni kuendeleza haya. Kama mambo haya yataendelezwa baada
ya uchaguzi, ni dhahiri kuwa mpira utazidi kuendelea. Hakuna njia ya mkato
katika maendeleo.”
Uchaguzi
wa TFF ulihusisha nafasi za rais, makamu wa rais na wajumbe wa Kamati ya
Utendaji kutoka Kanda 13 za Shirikisho.
No comments:
Post a Comment