Uchaguzi Mkuu wa TFF, TPL wasitishwa
Na Mwandishi Wetu
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Kandanda Nchini (TFF) imesitisha uchaguzi mkuu wa Shirikisho hilo na Bodi ya Ligi (TPL) kwa muda usiojulikana kutokana kwa sababu za kikanuni.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deogratias Lyatto alisema kuwa moja ya sababu hizo ni muda wa kampeni kwa chaguzi zote mbili kwani wagombea wanatakiwa kufanya kampeni kwa siku tano, jambo ambalo haliwezekani kwa hali ya sasa.
Lyatto alisema kuwa hali hiyo inatokana na kuomba kwa marudio ya hukumu kwa wagombea wawili, Jamal Malinzi kwa upande wa nafasi ya Urais wa TFF na Ahmad Yahya kwa upande wa nafasi ya Uenyekiti kwa upande wa TPL kwa kamati ya Rufaa ambayo haijakutana kutoa maamuzi yao.
Alisema kuwa endapo maamuzi hayo yataolewa kesho au siku yoyote, muda wa kampeni kwa wagombea utakuwa kinyume na kanuni za uchaguzi na hivyo 'kukiuka kanuni hizo'.
Kwa upande wa bodi ya Ligi, Lyatto alisema kuwa kampeni kwa wagombea wa uchaguzi huo zilipaswa kuanza leo (Februari 17), lakini kutokana na maombi ya marejeo ya hukumu ya Yahya, mgombea hataweza kupata muda wa siku tano wa kampeni.
Alifafanua kuwa kwa mujibu wa Ibara ya 10 (5), kamati yake imepewa mamlaka ya kutoa maamuzi hayo ili kukidhi matakwa ya kanuni na tarehe mpya ya chaguzi zote zitatangazwa hapo baadaye.

Deogratias Lyatto

No comments