Juma Kaseja |
Mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam
jana, Simba walibanwa na wageni na kuruhusu bao pekee katika mchezo huo
lililofungwa dakika ya 24 na Joao Martins kwa kichwa akiunganisha mpira wa
krosi uliopigwa na Carlos Almeida.
Simba ambao walianza mchezo kwa hofu huku wakiwaacha wageni
kuutawala, ambapo dakika ya saba wanaonana vizuri na Sidnei Mariano alipiga
shuti kali lililogongwa mwamba wa goli la Simba na kurudi uwanjani.
Dakika ya 13, Simba walipata nafasi nzuri ya kufunga bao, lakini mpira
wa krosi uliopigwa na Nassor Chollo unakosa
mmaliziaji na kuwapa nafasi mabeki wa Libolo kuondosha hatari langoni kwao.
Libolo wakicheza kwa kujiamini, akili na nguvu waliwadhibiti vizuri
washambuliaji wa Simba, Mrisho Ngassa na Haruna Moshi ‘Boban’, ambao walikuwa
wakipelekwa pembeni mara kwa mara.
Dakika moja kabla ya mapumziko, kipa wa Simba, Juma Kaseja,
alifanya kazi kubwa ya kuokoa shuti kali la Carlos Almeida lililokuwa
likielekea wavuni.Simba walikosa bao la kusawazisha dakika ya 64, baada ya Boban,
kushindwa kutumia vizuri pasi iliyotoka kwa Haruna Chanongo, wakati tayari
mpira ukiwa umewapita mabeki wa Libolo.Beki aliyerejeshwa kundini Simba, Juma Nyosso, alijaribu kwenda
mbele na kufanya shambulizi la nguvu, lakini shuti lake la mguu wa kushoto
lilipaa juu ya lango la wapinzani wao.
Kwa matokeo hayo, Simba imejiweka katika nafasi ngumu ya kusonga
mbele kwenye michuano hiyo, kwani watakuwa na kibarua kigumu katika mechi ya
marudiano itakayopigwa wiki mbili zijazo nchini Angola.Simba: Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Nassor Chollo,
Koman Billi Keita, Juma Nyosso, Mussa Mude/Amir Maftah, Haruna Chanongo/Ramadhan
Singano, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Haruna Moshi ‘Boban/Salim Kinje, Mrisho
Ngassa.
Libolo: Landu Mavanga, Carlos Almeida, Antonio Cassule, Pedro
Ribeiro,Gamaliel Musumari, Manuel Lopez, Sidnei Mariano, Dorivaldo Dias, Joao
Martins/Andres Madrid, Dorio Cardoso, Maieco Antonio/Herry Camara.
No comments:
Post a Comment