![]() |
Frank Lampard (kushoto) na John Terry |
Chelsea, jana iliibuka na ushindi wa mabao 4-0,
katika mechi ya kuwania kombe la FA raundi ya tano iliyochezwa kwenye Uwanja wa
Stamford Bridge, jijini London.
Juan
Mata aliifungia Chelsea bao la kwanza dakika ya 54, baada ya kipindi cha kwanza
kumalizika wakiwa hawajafungana.
Chelsea
walijipatia bao la pili dakika ya 68, kupitia kwa Oscar baada ya kupiga shuti kali lililomgonga
Simon Moore na kujaa wavuni.
Frank
Lampard, ambaye ataweza kuondoka katika timu hiyo, aliifungia bao la tatu Chelsea,
akitumia vizuri mpira wa krosi uliopigwa na Oscar na kujaa wavuni.
Beki
aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu, John Terry, aliifungia timu yake bao la nne
kwa kichwa, akitumia vizuri mpira wa krosi wa Oscar.
No comments:
Post a Comment