Waziri Kawambwa amwaga vifaa Bagamoyo
![]() |
Waziri Shukuru Kawambwa |
WAZIRI wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dk
Shukuru Kawambwa, ametoa vifaa mbalimbali vya michezo kwa madiwani wa jimbo la
hilo.
Kawambwa
ametoa vifaa hivyo ikiwa ni moja ya njia za kuhamasisha ushiriki wa timu katika
michuano ya kombe la madiwani hao katika kata saba za jimbo hilo.
Akizungumza
katika hafla fupi ya kuwakabidhi vifaa hivyo, Dk Kawambwa alisema kuwa, ameamua
kutoa msaada huo wa vifaa kwa lengo la kuwasaidia madiwani hao ili waweze
kuendesha michuano kwa timu kutoka katika kata zao.
Alisema
vifaa hivyo vitazisaidia timu zao ambazo ndio washiriki wa michuano ya Kombe la
Kawambwa ambayo hufanyika kila mwaka wilayani humo.
“Kwa
ujumla napenda kuwashurukuru madiwani hawa kwanza kwa kuniunga mkono katika
michuano iliyopita lakini kubwa zaidi kazi nzuri waliyoifanya kwa ushirikiano mkubwa
na kamati yangu ya jimbo.
“Kwa
jumla ya miaka yote saba mbapo michuano hii imechezwa madiwani mmeweza
kusimamia vizuri na kuleta changamoto kubwa katika michezo,” alisema Kawambwa
Akizungumzia
mafanikio ya michuano hiyo, Kawambwa alisema kuwa michuano hiyo ya madiwani na
hatimaye “Kawambwa Cup” imekuwa na mafanikio makubwa kwa vijana wilayani Bagamoyo
kwani wengi wao wameweza kupata nafasi za masomo na wengine kusajiliwa na timu
kutoka mikoa mingine nchini.
Alisema
kuwa lengo kubwa la kuwapo kwa mashindano kama hayo ni kutaka kuwahamasisha
vijana kuona kuwa michezo inaweza kutumika kama ajira mbadala hata kwa vijana
ambao hawana elimu kutokana na matatizo mbalimbali.
Alisema
kuwa michuano ya Kawambwa Cup mwaka huu inatarajiwa kugharimu Sh. milioni 28, tofauti
na ile ya mwaka jana ambayo ilitumia Sh. Milioni 26 na imekuwa ikidhamini kwa
ushirikiano mkubwa baina ya ofisi yake na kampuni ya Tanzania Distrlies Limited
watengenezaji wa Konyagi.
No comments