VPL 2012/2013 KUANZA KUTIMUA VUMBI KESHO
Michuano
ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara 2012/2013 inaanza
kutimua vumbi kesho (Septemba 15 mwaka huu) ambapo timu zote 14 zitakuwa kwenye
viwanja saba tofauti.
Mabingwa
watetezi Simba wataikaribisha African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam. Mjini Morogoro, Polisi Dodoma watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar kwenye
Uwanja wa Jamhuri wakati jijini Tanga, Mgambo JKT ambayo imepanda daraja msimu
huu itaumana na Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
Tanzania
Prisons ambayo nayo imerejea VPL msimu huu itaialika Yanga kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. JKT Ruvu na Ruvu Shooting zitapambana
kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam huku Azam ikiwatembelea
Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Katiba.
Uwanja
wa CCM Kirumba jijini Mwanza utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Toto Africans
dhidi ya Oljoro JKT. Mechi zote zitaanza saa 10.30 jioni.
Viingilio
katika mechi ya Simba na African Lyon vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya
kijani na bluu, sh. 8,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 viti vya VIP C
na B wakati VIP A itakuwa sh. 20,000. Viingilio kwa mechi nyingine vitakuwa sh.
3,000 na sh. 10,000.
No comments