Simba kumpeleka Yondani Polisi
![]() |
Kelvin Yondan |
KAMATI ya Utendaji ya klabu ya Simba,
imeamua kupeleka saini ya kidole katika jeshi la Polisi ili kubaini saini
halali ya mchezaji Kelvin Yondani, ambaye ameidhinishwa kuichezea timu ya Yanga
katika ligi kuu Tanzania Bara.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema maamuzi hayo yametolewa juzi, katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, na kuamua kutulipia mbali maamuzi ya kususia Ligi Kuu na michuano yoyote ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Alisema kuwa, kufuatia
maamuzi ya kikao cha Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF,
kilichokaa Jumatatu iliyopita kujadili hatma ya wachezaji Kelvin Yondani na
Mbuyu Twite, kamati ya utendaji ya klabu hiyo, ilikutana siku mbili mfululizo,
Septemba 11 na 12, na kufikia maamuzi hayo.Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema maamuzi hayo yametolewa juzi, katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, na kuamua kutulipia mbali maamuzi ya kususia Ligi Kuu na michuano yoyote ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kamwaga alisema kuwa, hata hivyo maamuzi hayo yametokana na busara za wazee wa klabu hiyo, ambao waliusihi uongozi na kamati ya utendaji, kuachana na maamuzi hayo.
Alisema kabla ya kutangaza maamuzi ya Kamati ya Utendaji, wanachama waandamizi wa klabu Samuel Sitta, Profesa Philemon Sarungi, Yusuf Makamba na Profesa Juma Kapuya, kwa mchango wao mkubwa wa kimawazo kwa kamati ya utendaji, ambayo yalikuwa na ushawishi mkubwa na kufikia maamuzi hayo.
Alisema kuwa, wazee wa klabu hiyo waliamua kuwaambia viongozi wa Simba, waachane na maamuzi hayo na kufuata taratibu husika.
Alisema kwamba, wanachama au wapenzi wote waliokuwa na nia ya kutaka kupeleka suala hili mahakamani, wasitishe dhamira yao, ikiwa suala hili litapelekwa mahakamani, klabu inaweza kuathirika kwa namna nyingi, ikiwamo kuzuiwa kushiriki mashindano yoyote yanayotambuliwa na TFF, CAF na FIFA.
Kamwaga alisema kuwa, kamati hiyo imaamua kulipeleka suala la Yondan katika Jeshi la Polisi, ambao wana vifaa maalum vya kugundua alama za vidole na sahihi.
Uongozi wa Simba utakuwa ukitoa taarifa za mara kwa mara zinazohusu masuala haya, na unawataka wanachama na wapenzi wake kutulia, wakati wakiendelea kuyashughulikia
Hata hivyo, alisema kamati hiyo imeamua kuwapa muda viongozi wa Yanga, kama ilivyosema Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji, kuwa fedha za klabu hiyo, zilipwe ndani ya siku 21.
Kamwaga alisema wanasubiri siku 21, zimetolewa na kamati ya Sheria, baada ya mchezaji Mbuyu Twite, kuidhinishwa kuichezea Yanga.
Alisema kuwa, Simba itashiriki mashindano yote ya TFF, ikianzwa na mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya African Lyon, itakayoanza kuchezwa kesho.
"Klabu ya Simba itashiriki mashindano yote ya TFF, lakini kwa sasa tunasubiria siku 21, walizopewa Yanga, na kamati ya Sheria kutulipa fedha zetu," alisema Kamwaga.
Ofisa Habari huyo wa Simba, aliwataka wapenzi wa klabu hiyo, wawe na mshikamano katika kuhakikisha klabu yao ikifanya vizuri katika mashindano mbalimbali itakayoshiriki.
No comments