Header Ads

ad

Breaking News

Luka Modric kupimwa afya Real Madrid leo


Luka Modric
 LONDON, England

Tottenham imekubali kuwauzia Real Madrid kiungo wao Luka Modric, ada ya puani milioni 30.  

Mchezaji huyo kutoka Croatia mwenye miaka 26, leo atakwenda Hispania kupimwa afya. 

Tottenham, pia imetangaza kuingia ushirikiano na klabu ya Real Madrid. 

Makubaliano hayo yatazifanya klabu hizo mbili kufanya kazi pamoja ikiwemo wachezaji , makocha na uhusiano wa kiabishara. 

Modric alijiunga Tottenham mwaka 2008 kwa pauni milioni 16.5, akitokea katika klabu ya Dinamo Zagreb ya Croatia.

No comments