KOMBAINI COPA COCA-COLA YAENDA AFRIKA KUSINI
![]() |
Msemaji wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo |
Kombaini
ya Copa Coca-Cola Tanzania (Dream Team) yenye wachezaji 16 inatarajia kuondoka
kesho (Agosti 28 mwaka huu) asubuhi kwenda Afrika Kusini kwenye kambi
itakayokuwa chini ya makocha wa Chelsea.
Makocha
watano kutoka timu ya Chelsea ya Uingereza ndiyo watakaoongoza kambi maalumu ya
kimataifa ya Copa Coca-Cola yenye wachezaji 140 kutoka nchini 15 itakayofanyika
jijini Pretoria kuanzia Agosti 28 hadi Septemba 8 mwaka huu.
Robert
Luke Udberg, Russel William Banyard, Oliver Staurt Woodall, Shane Jason Hughes
na Dean Aaron Steninger kutoka Chelsea FC Foundation ndiyo wanaounda jopo hilo
la makocha litakalowanoa vijana hao wenye umri chini ya miaka 17.
Wachezaji
wanaounda Dream Team iliyotokana na michuano ya Copa Coca-Cola iliyofanyika
jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 24 hadi Julai 15 mwaka huu ni Abrahman Said
Mohamed (Zanzibar), Ayubu Alfan (Dodoma), Baker Hamad (Tanga), Edward Joseph
(Ruvuma), Hassan Kabunda (Temeke) na Joseph Chidyalo (Dodoma).
Wengine
ni Mtalemwa Katunzi (Morogoro), Mwarami Maundu (Lindi), Nankoveka Mohamed
(Ilala), Nelson Peter (Morogoro), Rajab Rashid (Mwanza), Said Ramadhan
(Kagera), Shiza Kichuya (Morogoro), Shukuru Msuvi (Temeke), Tanganyika Suleiman
(Kigoma) na Tumaini Baraka (Kilimanjaro).
Nchi
nyingine zitakazokuwa na washiriki katika kambi hiyo ni wenyeji Afrika Kusini,
Burundi, Cameroon, Congo Brazzaville, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC),
Kenya, Lesotho, Malawi, Msumbiji, Nigeria, Swaziland, Uganda, Zambia na Zimbabwe.
Hii
ni mara ya sita mfululizo kwa kampuni ya Coca-Cola kupeleka Dream Team kwenye
kambi za kimataifa. Mwaka 2007 na 2008, timu hiyo ilikwenda Brazil wakati mwaka
2009, 2010 na 2011 ilikuwa Afrika Kusini.
No comments