HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE AKIZINDUA AWAMU YA TATU YA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII (TASAF III) UWANJA WA JAMHURI, DODOMA, 15 AGOSTI 2012
Mhe. Spika;
Mhe. Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar;
Mhe. Steven Wassira, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Uratibu na
Mahusiano,;
Waheshimiwa Mawaziri;
Mhe. Daktari Rehema Nchimbi, Mheshimiwa Steven Wassira (Mb);
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma;,
Mheshimiwa Dr. Rehema Nchimbi;
Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge;
Mhe. Katibu Mkuu Kiongozi;
Mwakilishi wa Benki ya Dunia: Tanzania, Uganda na Burundi,
Bwana Philippe Dongier;
Ndugu Peniel Lyimo, Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi wa
TASAF;
Mwakilishi wa Benki ya Dunia;
Wawakilishi wa Ndugu Peniel Lyimo;
wWashirika wetu wangine wa mMaendeleo; ,
Waheshimiwa Viongozi wa Vyama vya Siasa;
Waheshimiwa Wabunge
Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa nawa Serikali;
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF;
Wageni wWaalikwa;
Mabibi na Mabwana:;:
Shukrani
Ndugu Wananchi:
Namshukuru sana Mheshimiwa Waziri Steven Wassira na Nndugu Ladislaus
Mwamanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na Kamati
yake kwa kunialika nije kushiriki nanyi kwenye uzinduzi wa Awamu ya Tatu ya
TASAF.Tarehe 30 Machi 2000 tulizindua Awamu ya Kwanza ya Mfuko wa Kwa kuwa huko
tulipotoka tumepata mafanikio ya kutia moyo, naomba nianze kwa kutoa pongezi na
kuwashukuru wote walioshiriki kufanikisha utekelezaji wa awamu mbili za TASAF
zilizotangulia.
Pongezi
Ndugu Wananchi;
Napenda kuishukuru kwa dhati Benki ya Dunia na Mwakilishi Mkazi wa Benki
hiyo wa wao hapa nchini kwa kushirikiana na sisi kutekeleza miradi mbalimbali ya
TASAF tangu mwaka 2000. Siku zote Benki ya Dunia imekuwa mwenzetu muhimu na wa
kutumainiwa na hii inasikiliza hoja zetu na kuzingatia vipaumbele vya sSerikali
na wananchi wa Tanzania yetu katika jitihada zetu za kupambana na umaskini na
kujiletea maendeleo. Tunafurahishwa sana na sera ya kusikiliza vipaumbele
vyetu. Jambo hilo Hali hii ndiylo limetuwezesha sisi kushirikiana nao kubuni
mpango huu wa TASAF unaofadhiliwa na ubia mzuri wa maendeleo kati yetu Serikali
na Benki ya Dunia, , kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo, Serikali
zetu mbili na wananchi wa nchi yetu.
Natoa ipongezai nyingi kwa sana Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF, chini
ya uenyekiti imara wa Ndugu Peniel Lyimo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa
uongozi wake thabiti wa kusimamia vizuri shughuli za TASAF. Aidha, nampongeza
Katibu Mkuu, Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa usimamizi wake
thabiti. Hali kadhalika nNawapongeza pia viongozi na watendaji katika
Halmashauri zote za Tanzania Bara , Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
kwa kazi nzuri waifanyayo ya usimamizi na utekelezaji wa miradi katika awamu
iliyotangulia. Bila uongozi wao thabiti, mafanikio ya Awamu zya Kwanza na Pili
yangekuwa ni ndoto. Kwa namna ya pekee nawapongeza wananchi wote walioitikia
wito na kuchangia kwa hali na mali kufanikisha utekelezaji wa mpango huo wa
kujiletea maendeleo yao wenyewe.
Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipoipongeza Kamati ya Dkt. Servacius
Likwelile, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, kwa kazi nzuri ya kuandaa Awamu
ya Tatu ya TASAF. Kazi hiyo wameifanya vizuri na kwa umakini mkubwa wahuku
akikishirikiana na Bibi Ida Manjolo na wataalamu wengine wa Benki ya Dunia.
Tunawashukuru sana.
Mabibi na Mabwana;
Kuna msemo wa Kiswahili usemao “ukiona vyaelea, ujue vimeundwa”. Na hivi
ndivyo ilivyo kwa TASAF. Siri ya mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa
Awamu ya Pili ni usimamizi mzuri unaofanywa na Menejimenti ya TASAF. Hivyo
napenda kuchukua nafasi hii kuipongeza Menejimenti, Mkurugenzi Mtendaji, na
wafanyakazi wote wa TASAF kwa kusimamia vizuri shughuli na miradi mbalimbali
iliyotekelezwa katika Awamu ya Pili. Ni matumaini yangu kuwa mtafanya vizuri
maradufu katika Awamu ya Tatu tunayoizindua leo.
Utekelezaji wa Awamu ya Pili ya TASAF
Ndugu Wananchi;
Utekelezaji wa Awamu ya Pili ya
TASAF ulikuwa na mafanikio makubwa. Jumla ya miradi 11,572 imetekelezwa na kati
ya hiyo, miradi 4,294 ilikuwa ya huduma za jamii; miradi 1,405 ya ujenzi na
miradi 5,875 ya makundi maalum. Miradi hiyo imegharimiwa na serikali kwa
kushirikiana na washirika wake wa maendeleo. Serikali imetoa Shillingi bilioni
32.2 na Benki ya Dunia ilitupatia mkopo wa masharti nafuu wa Shilingi bilioni
322. Washirika wetu wengine walituongezea nguvu kwa kuchangia Shillingi bilioni
72. Aidha, wananchi wametoa fedha, rasilimali na nguvu kazi ambazo thamani yake
inakadiriwa kuwakwa ujumla ni zaidi ya Shilingi billioni 20.2.
Miradi ya Huduma
Miradi ya Huduma za Jamii imeongeza na/au kuboresha madarasa 5,485; ofisi
za walimu 150; nyumba za walimu 152;, maabara kwenye shule za sekondari 157;
majengo ya utawala katika shule za sekondari 20; mabweni ya wanafunzi 163; vyoo
vya wanafunzi 705; madawati 22,946, viti 5,483, meza 4,354; vituo vya afya 63;
zahanati 606, nyumba za watumishi wa zahanati 301, vyoo kwenye zahanati 339,
vichomea taka 182; vituo vya maji 2,198, visima virefu 192, visima vifupi 335 na
matanki ya maji 205.
Miradi ya Ujenzi
Miradi ya ujenzi, yenyewe
imeongeza au kuboresha barabara za vijijini 825; mabwawa madogo 78; mifumo
midogo ya umwagiliaji 289; mifumo ya kuondoa maji ya mvua barabarani mita 4,593;
maghala ya kuhifadhia nafaka 113; masoko 80; makaravati 901; madaraja ya
watembea kwa miguu 64; na, miradi ya mazingira 608 yenye walengwa 566,938.
Makundi Maalum
Na miradi ya makundi maalum imetoa huduma kwa yatima 32,113; wajane 15,205;
wazee 17,961; watu wenye ulemavu 7,840; watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI
52,316; na vijana wasio na ajira 36,859. Vilevile, watu 2,083 wamehamasishwa
kujikinga na ugonjwa wa UKIMWI.
Mabibi na Mabwana;
Mafanikio ya utekelezaji wa
Awamu ya Pili ya TASAF hayakuishia hapo. Vikundi 1,778 vyenye wanachama 22,712
vimeundwa kupitia Mpango wa Kuweka Akiba na Kuwekeza (COMSIP ) katika
Halmashauri 44 zilizopo Tanzania Bara, Unguja na Pemba. Walengwa wote wamepatiwa
mafunzo ya kuendesha vikundi vyao kwa ufanisi pamoja na vifaa. Vilevile, mafunzo
ya usimamizi, utekelezaji bora wa miradi na fani mbalimbali katika ngazi ya
vijiji, wilaya na taifa yametolewa kwa walengwa 27,373.
Serikali kupitia TASAF
imefanikiwa pia kutekeleza Programu ya Kijamii ya Uhawilishaji Fedha kwa Kaya
Maskini kwa majaribio katika Wilaya za Bagamoyo, Kibaha na Chamwino. Walengwa
zaidi ya 13,000 kutoka kaya 6,000 maskini na zilizo katika mazingira hatarishi
zilipatiwa ruzuku ya jumla ya shillingi bilioni moja na nusu. Kaya hizo
zimejengewa uwezo na watoto sasa wanapelekwa kwenye zahanati na vituo vya afya
kwa ajili ya chanjo na kufuatiliwa maendeleo yao.
Aidha, watoto 1,638 ambao
hawakuweza kwenda shule kwa sababu ya umasikini sasa wameandikishwa na
wanakwenda shule. Kati ya wanafunzi hao, 392 wamefaulu kwenda shule za sekondari
za kata. Vile vile wazee 4,956 wamewezeshwa kupata huduma za afya na baadhi yao
wamejiunga na bima ya afya ili kupata huduma kwa urahisi na uhakika zaidi.
Kufuatia mafanikio ya haraka ya programu hii, sasa maandalizi yanafanyika ili
isambazwe kwenye Halmashauri zote katika utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya
TASAF.
Ndugu Wananchi;
Inafurahisha kuona jinsi suala
la jinsia lilivyozingatiwa katika utekelezaji wa programu na miradi ya TASAF.
Wanaume na wanawake walishirikishwa sawa sawa katika hatua zote za utekelezaji
wa miradi yao. Idadi ya wanawake katika kamati ya mradi ilipangwa makusudi ili
isipungue asilimia 50 ya jumla ya wajumbe, na idadi ya walengwa wanawake katika
miradi ya ujenzi nayo isipungue asilimia 50. Bahati nzuri akina mama waliokuwa
wajumbe kwenye Kamati mbalimbali wameonesha uwezo mkubwa wa uongozi. Naomba
ushirikishwaji huu uendelee kuimarishwa na akina mama wajitokeze kwa wingi
kushiriki katika usimamizi wa miradi ya TASAF ya Awamu ya Tatu.
Ni wazi kuwa siri ya mafanikio ya Awamu ya Pili ya TASAF ni ushiriki mzuri
wa wananchi, utayari wao wa kumiliki maendeleo yao wenyewe na moyo wa kujituma
kwao pamoja na uongozi na usimamizi mzuri wa miradi katika ngazi zote.
Changamoto Katika Utekelezaji wa Awamu ya Pili
Maendeleo ya Jamii (TASAF I) kule Mwanhuzi, Wilayani Meatu, Mkoa wa
Shinyanga.
Vile vile tarehe 23 Mei 2005, tulizindua Awamu ya Pili ya Mfuko huu (TASAF
II ) kule Wilayani Magu, Mkoa wa Mwanza.
Leo hii ninayo furaha kubwa kuja hapa Dodoma kuzindua Awamu ya Tatu ya
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF III).
Tunazindua Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii kwa kuwa Awamu ya
Kwanza na ya Pili zimetekelezwa kwa mafanikio makubwa. Hivyo basi, naanza kwa
kutoa shukurani na pongezi zangu za dhati kwa wote walioshiriki kufanikisha
Awamu mbili zilizotangulia na walioshiriki kuandaa Awamu hii ya Tatu.
Naishukuru Benki ya Dunia na ninamshukuru Mkurugenzi Mwakilishi wa Benki
hii kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi, Bw. Philippe Dongier. Kwa hakika
Bw. Dongier anaiwakilisha vyema Benki ya Dunia ambayo siku zote inasikiliza hoja
na kuzingatia vipaumbele vya vita dhidi ya umaskini vinavyowekwa na Serikali
yetu. Mfano halisi ni Mfuko huu wa Maendeleo ya Jamii - TASAF. Kwa usikivu
huo, tumebuni ubia mzuri wa maendeleo kati ya Serikali yetu, Benki ya Dunia,
Wadau wengine wa Maendeleo na Wananchi.
Napenda pia, kuwashukuru washirika wengine wa maendeleo ambao wanashiriki
Awamu hii ya Tatu ya TASAF hususan Serikali ya Uingereza kupitia Idara yake ya
Maendeleo ya Kimataifa (DFID), Serikali ya Hispania na Serikali ya Watu wa
Marekani kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa (USAID).
Ninawashukuru Wataalam wa Benki ya Dunia na Washirika wengine wa Maendeleo
wakiongozwa na Bibi Ida Manjolo ambao walishirikiana nasi kwa karibu katika
utekelezaji wa Awamu ya Pili ya TASAF na kuandaa Awamu ya Tatu.
Naipongeza pia Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF ambayo mwenyekiti wake
ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ndugu Peniel M. Lyimo, pamoja na Kamati
ya Maandalizi ya Awamu ya Tatu ya TASAF iliyoongozwa na Naibu Katibu Mkuu,
Wizara ya Fedha, Dkt. Servacius B. Likwelile, kwa kazi nzuri.
Nawapongeza Viongozi na Watendaji katika Halmashauri zote za Tanzania Bara,
Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na wananchi wote kwa jumla kwa
usimamizi na utekelezaji wa miradi ya jamii katika awamu zote mbili
zilizotangulia. Wananchi wote waliitikia kwa moyo mkunjufu na ari kubwa kupokea
mawazo ya Serikali katika utekelezaji wa mpango huo wa kujiletea maendeleo yao
wenyewe.
Naipongeza pia Menejimenti ya TASAF, ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji,
Ndugu Ladislaus J. Mwamanga na wasaidizi wake. Nina imani kuwa wataendelea
kufanya kazi nzuri katika Awamu hii ya Tatu.
Tangu mwaka 2000 TASAF imekuwa ni kichocheo katika jitihada za wananchi
kujiletea maendeleo. TASAF haina miradi; miradi ni ya wananchi. Inachokifanya
TASAF ni kuwawezesha tu wananchi kutekeleza vipaumbele vyao vya maendeleo.
Awamu ya Pili ya TASAF iligharimiwa kwa kiasi kikubwa na mkopo wa masharti
nafuu kutoka Benki ya Dunia. Mkopo huo ni kiasi cha Shilingi 322 bilioni sawa
na Dola za Kimarekani 215 milioni. Vilevile kwa utekelezaji mzuri wa TASAF,
kumekuwa na Wahisani na Miradi mingine kupitishia fedha TASAF zenye jumla ya
shilling 72 bilioni sawa na Dola za Kimarekani 45 milioni. Mchango wa Serikali
yetu ulikuwa ni Shilingi 32.2 bilioni, na wananchi walichangia fedha rasilimali
na nguvu kazi ambazo thamani yake ilifikia zaidi ya Shilingi 20.2 bilioni.
Ndugu Wananchi
Ushiriki wa wananchi, utayari wao wa kumiliki maendeleo yao na kujituma
kwao pamoja na uongozi na usimamizi mzuri wa kitaifa na halmashauri husika ndio
msingi wa mafanikio ya Awamu ya Pili ya TASAF.
Mafanikio hayo ni pamoja na :-
1.Jumla ya miradi 11,572 ilipitishwa na kupewa fedha; miradi 4,294 ikiwa ya
Huduma za Jamii, miradi 1,405 ya Ujenzi na miradi 5,875 ni ya Makundi
Maalum.
2.Miradi ya Huduma za Jamii imeongeza na/au kuboresha madarasa 5,485, ofisi
za walimu 150, nyumba za walimu 152, maabara kwenye shule za sekondari 157,
majengo ya utawala katika shule za sekondari 209, mabweni ya wanafunzi 163, vyoo
vya wanafunzi 705, madawati 22,946, viti 5,483, meza 4,354; zahanati 606, vituo
vya afya 63, nyumba za watumishi wa zahanati 301, vyoo kwenye zahanati 339,
vichomea taka 182; vituo vya maji 2,198, visima virefu 192, visima vifupi 335 na
matanki ya maji 205.
3.Miradi ya ujenzi imeongeza au kuboresha barabara za vijijini 825, mabwawa
madogo 78, na mifumo ya kuondoa maji ya mvua barabarani mita 4,593, maghala ya
kuhifadhia nafaka 113, masoko 80, mifumo midogo ya umwagiliaji 289, makaravati
901, miradi ya mazingira 608 yenye walengwa 566,938 na madaraja ya watembea kwa
miguu 64.
4.Miradi ya makundi maalum imetoa huduma kwa yatima 32,113, wajane 15,205,
wazee 17,961, watu wenye ulemavu 7,840, watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI
52,316 na vijana wasio na ajira 36,859. Vilevile, uhamasishaji juu ya kudhibiti
UKIMWI umetolewa kwa watu 2,083.
5.Vikundi 1,778 vyenye wanachama 22,712 vimeundwa kupitia Mpango wa Kuweka
Akiba na Kuwekeza (COMSIP ) katika Halmashauri 44 na Unguja na PembaWalengwa
wote wamepatiwa mafunzo ya kuendesha vikundi vyao kwa ufanisi pamoja na
vifaa.
6.Mafunzo ya usimamizi, utekelezaji bora wa miradi na fani mbalimbali
katika ngazi ya vijiji, wilaya na taifa yametolewa kwa walengwa mbalimbali
27,373.
Ndugu wananchi,
7.Serikali pia kupitia Awamu ya Pili ya TASAF imefanikiwa kutekeleza
Programu ya Kijamii ya Uhawilishaji Fedha kwa Kaya Maskini kwa majaribio katika
Wilaya za Bagamoyo, Kibaha na Chamwino. Walengwa zaidi ya 13,000 kutoka kaya
6,000 maskini na zilizo katika mazingira hatarishi zilipatiwa ruzuku ya jumla ya
shillingi bilioni moja na nusu (Sh. 1,500,000,000). Kaya hizo zimejengewa
uwezo na watoto ambao ndiyo walengwa wanapelekwa kwenye zahanati na vituo vya
afya kwa ajili ya chanjo na kufuatilia maendeleo yao.
8.Aidha, watoto 1,638 ambao hawakuweza kwenda shule sababu ya umasikini
sasa wameandikishwa na wanakwenda shule. Kati ya wanafunzi hao 392 wamefaulu
kwenda shule za sekondari za kata. Vile vile wazee 4,956 ambao ni walengwa
wamewezeshwa kupata huduma za afya. Pia Kaya za walengwa zimejiunga na mpango
wa bima ya afya ili kupata huduma kwa urahisi na uhakika zaidi.
9.Programu hii imekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha hali ya maisha ya
kaya za walengwa kwa muda mfupi sana. Mafanikio yake yamefanya sasa programu hii
kusambazwa kwenye Halmashauri zote katika utekelezaji wa TASAF Awamu ya Tatu.
Haya yote yasingewezekana bila ninyi wananchi kukubali kwa pamoja kushiriki
katika kurekebisha hali ya uchumi wetu, kwa kuwa muhimili mkuuwa maendeleo
katika ngazi ya jamii.
Ndugu wananchi,
Kwa kuwa TASAF imepanua uwigo wa kuwafikia walengwa masikini katika makundi
mbalimbali ndani ya Tanzania Bara na Zanzibar na uzoevu wao wa zaidi ya miaka
kumi na mbili; ni dhahili kuwa ni chombo pekee cha serikali chenye uwezo wa
kutekeleza vizuri Mpango wa Kitaifa wa Kinga ya Jamii ( National Social
Protection Framework)
Awamu ya Pili ya TASAF imeimarisha uwajibikaji katika ngazi zote kwa
kuhakikisha kuwa fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli
mbalimbali zinatolewa taarifa na wadau wote wanajulishwa mapato na matumizi
yake. Kamati za usimamizi wa miradi ziliwajibika kutoa taarifa za utekelezaji
hatua kwa hatua na matumizi ya fedha.
Suala la jinsia katika utekelezaji wa miradi lilizingatiwa, na kuonekana
wazi kuwa ni jambo la haki na la manufaa kila palipokuwa na mradi unaochangiwa
na TASAF. Wanaume na wanawake walishirikishwa sawa sawa katika hatua zote za
utekelezaji wa miradi yao. Idadi ya wanawake katika kamati ya mradi ilipangwa
kwa makusudi isipungue asilimia 50 ya jumla ya wajumbe, na idadi ya walengwa
wanawake katika miradi ya ujenzi nayo isipungue asilimia 50. Lengo ni
kuhakikisha kuwa kipato kisichopungua asilimia 50 kinaelekezwa kwa walengwa
ambao ni wanawake. Matumaini yangu ni kuwa uwezo waliouonyesha wanawake
waliokuwa kwenye kamati hizi utawasukuma wengi wao kuomba uongozi katika ngazi
mbalimbali.
Ndugu wananchi;
Pamoja na mafanikio hayo ya kutia moyo, Wakati wa utekelezaji wa Awamu ya
Pili ulikabiliwa na changamoto ya TASAF kumekuwepo na changamoto mbalilmbali.
Changamoto hizo ni pamoja na uhaba wa fedha kutokutosheleza kukidhi wezo wa
Mfuko kutokidhi mmahitaji ya wananchi; uwezo mdogo wa kusimamia miradi katika
ngazi mbalimbali za uongozi; na ya wananchi ambayo ni mengi, ukosefu wa huduma
kwenye baadhi ya vituo vya kutolea huduma kama zahuhaba wa watumishi katika
vituo vya kutoa huduma. Bahati nzuri serikali na uongozi wa TASAF unazitambua
changamoto hizo na tumejipanga vizuri kukabiliana nazo katika Awamu hii ya Tatu
tunayoizindua leo.
Awamu ya Tatu ya TASAF
anati, vituo vya afya na masoko vilivyotokana na miradi kutokana na sababu
mbalimbali kama vile uhaba wa watumishi.
Changamoto nyingine ni pamoja uhaba wa fedha za utekelezaji wa shughuli za
kujenga uwezo, wigo mdogo wa utekelezaji wa jitihada nyingine, kama vile Mpango
wa Jamii wa Uhawilishaji Fedha kwa Kaya Maskini, Mpango wa Jamii wa Kuweka Akiba
na Kuwekeza, uansishwaji wa Taasisi za Maendeleo ya Jamii katika sehemu za
mijini.
Kadhalika ilijitokeza changamoto ambapo baadhi ya wanasiasa walipotosha
dhana ya kuanzishwa kwa TASAF na pia kutokuwepo mfumo wa uendelevu thabiti wa
kutekeleza TASAF kwa kutegemea rasilimali za ndani.
Mabibi na Mabwana;Ndugu wananchi
Kufuatia mafanikio katika utekelezaji wa Awamu mbili zilizotangulia na pia
katika kukabiliana na changamoto zake, Serikali imeamua kuanzisha Awamu ya Tatu
ya TASAF itatekelezwa kwa miaka kumi, katika vipindi viwili vya miaka mitano
mitano. ambapo Muondo wake umezingatia kupata ufumbuzi wa chanamoto
zilizopatikana na hivyo ambayo itatekelezwa katika kipindi cha miaka kumi nchi
nzima kwa Awamu mbili za miaka mitano mitano.
Tunategemea
Awamu hii ya Tatu ya TASAF itatoa mchango mkubwa katika kufikia nalenga
kuchangania kufikiwa malengo yetu yaliyomo kwenye ya D Dira ya Maendeleo ya
Taifa 2025, Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano, Mkakati wa Pili wa Kukuza
Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA II) na Mkakati wa Pili wa Kukuza Uchumi
Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Zanzibar (MKUZA II) na Mpango wa Mpango wa
Maendeleo wa Miaka Mita. Tutaweka mkazo zaidi katika miradi ya huduma za elimu,
afya na maji nay a kuondoa umaskini wa kipato. no kwa kuwekeza katika kuendeleza
rasilimali watu miongoni mwa kaya maskini na zilizo katika mazingira hatarishi.
Kupitia utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya TASAF tunatarajiainatarajiwa kuwa kaya
nyingimaskini maskini zitapiga hatua na kutoka kwenyekuanza kutoka katika
umaskini namaisha ya utegemezi. hatimaye kuwa na mchango katika kukuza uchumi
na kuondokana na utegemezi.
Ili kutekeleza miradi ya Awamu
ya Tatu ya TASAF, jumla ya Shilingi bilioni 408 zitahitajika. Fedha hizo
zitatolewa na serikali yetu, Benki ya Dunia na washirika wengine wa maendeleo.
Serikali itatoa Shillingi bilioni 45; Benki ya Dunia itachangia Shillingi
bilioni 330; Hispania itatoa Shillingi bilioni 9; Uingereza Shillingi bilioni
24; na Marekani Shillingi bilioni 1.4. Kama ilivyokuwa kwa Awamu zilizotangulia,
tunawategemea sana wananchi kutuunga mkono na kuchangia kwa hali na mali.
Mafanikio ya Awamu hii yatategemea sana mchango wa wananchi katika maeneo
husika.
Ahadi na Wito kwa Wananchi
Ndugu wananchi;
Tunapenda kuahidi kuwa tutaendelea kushirikiana na wananchi wote ambao
wanaonesha dhamira ya dhati ya kupambana na umaskini na kujiongezea
Kwa ushirikiano wenu wananchi, TASAF imetekelezwa vizuri sana na matunda
yake yapo wazi, na kwa vile mmeendelea kuiunga mkono Serikali yenu ya CCM katika
kutekeleza Mwelekeo wa Sera zake za Miaka mitano (2010-2015) zinazohimiza
mageuzi ya kiuchumi na uwezeshaji wananchi, serikali imetenga fedha tena na
kupata mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia na washirika wengine wa
maendeleo ili kutekeleza Awamu ya Tatu ya TASAF.
Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Dunia iliridhia na kupitisha utekelezaji wa
Awamu ya Tatu ya TASAF tarehe 29 Machi, 2012. Mkataba kati ya Benki ya Dunia na
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulisainiwa tarehe 15 Juni 2012. Na
idhini ya kuanza kutumia fedha hizo tayari imeshatolewa.
Awamu ya Tatu ya TASAF inatarajiwa kugharimu Shilingi 408 Bilioni sawa na
Dola za Kimarekani 272 Milioni kwa mchanganuo ufuatao:
1.Benki ya Dunia itachangia shilingi 330 bilioni (USD 220 milioni),
2.Serikali ya Hispania itachangia Shilingi 9 bilioni (USD 6 milioni)
3.Serikali ya Uingereza kwa kupitia Idara ya Serikali ya Uingereza ya
Maendeleo ya Kimataifa(DFID) itachangia Shilingi 24 bilioni (USD 16
milioni)
4.Serikali ya Watu wa Marekani kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya
Kimataifa (USAID) itachangia Shillingi 1.44 bilioni ( USD 900,000)
5.Serikali ya Tanzania itachangia sh.45 bilioni (USD 30 milioni)
Ndugu wananchi
Utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya TASAF unategemewa kuwa na changamoto
zifuatazo:
1.Upatikanaji wa raslimali fedha za kukidhi mahitaji halisi ya walengwa.
Jitihada za kupata rasilimali zaidi ziendelee na Wadau wa Maendeleo watoe
ushirikiano zaidi hasa wale ambao wameonyesha nia ya kushiriki katika kuchangia
mfuko huu.
2.Kujenga uwezo mapema wa kusimamia na kutekeleza kwa wakati uhawilishaji
wa fedha kwa walengwa. Mpango wa kujenga uwezo wa watekelezaji katika ngazi
mbalimbali upewe kipaumbele. Ufuatiliaji na tathmini vifanyike ili kubaini
mapungufu mapema iwezekanavyo.
3.Uwezo wa kusimamia utekelezaji miradi kwa ufanisi na kwa wakati. Ngazi
zote zinazohusika na utekelezaji zishiriki kikamilifu katika kuhakikisha
usimamizi wa utekelezaji unafanyika ipasavyo. Aidha, utekelezaji ufanyike kwa
awamu kuzingatia uwezo unavyojengwa.
4.Kusimamia uendelevu wa rasilimali na vituo vya kutolea huduma
vilivyotokana na miradi iliyotekelezwa na wananchi. Wataalamu kutoka halmashauri
husika na Viongozi katika maeneo ya utekelezaji wawezesha jamii kuwa na mipango
endelevu ya uendeshaji.
5.Usimamizi wa fedha zitakazotolewa kutekeleza miradi inayochangiwa na
TASAF utahitaji uwepo wa udhibiti mkubwa katika ngazi zote. Kazi hiyo nayo
ifanywe kuanzia sasa na kwa kipindi chote cha utekelezaji.
Ndugu wananchi,
Leo tunapozindua Awamu ya Tatu ya TASAF napenda tujikumbushe kuwa historia
yetu ya vita dhidi ya umaskini imetufundisha mambo kadhaa:
Kwanza, sera nzuri, mipango mizuri na nia njema peke yake havileti
maendeleo.
Pili, fedha za Serikali, mikopo au wahisani peke yake hazileti
maendeleo.
Tatu, ipo tofauti kubwa kati ya kutamani maendeleo na kuwa tayari
kutoka jasho kutafuta maendeleo.
Baada ya miaka 50 ya Uhuru sasa nadhani tumeelewa kunahitajika nini ili
maendeleo yaje kwa kasi ya kutosha kuweza kupunguza na hatimaye kuondoa umaskini
kabisa.
Hatua ya kwanza ya maendeleo ni mtu kutoridhika na hali duni ya maisha
yake; ni kujenga tamaa na wivu wa maendeleo na kuchukia hali ya umaskini.
Hatua ya pili ni mtu kuamua kwa dhati kutafuta maendeleo kwa jasho
lake, na inapobidi kwa kushirikiana na wenzake wanaochukia umaskini kama
yeye.
Hatua ya tatu ni mtu kupima uwezo alionao – uwezo wa fedha na wa mali
nyingine; uwezo wa akili na maarifa; na uwezo wa nguvu za kufanya kazi na kubuni
mbinu za kutumia ili kuboresha hali yake ya maisha na hali ya jamii yake kwa
ujumla.
Hatua ya nne ni kutekeleza kwa kadri ya uwezo wake mbinu za maendeleo
alizozibuni, au zilizobuniwa na jamii yake.
Hatua ya tano ni kuomba msaada kwa yale mambo yaliyo nje ya uwezo wake,
ikiwemo msaada wa fedha, msaada wa vifaa, au msaada wa elimu na utaalamu.
Mfuko huu wa Kuongeza Uwezo wa Wananchi katika Maendeleo ni jitihada
nyingine ya Serikali kuwasaidia wale wananchi ambao wamepitia hatua zote hizo za
kutafuta maendeleo, yaani tayari wameonyesha chuki yao dhidi ya umaskini,
wameamua kwa dhati kuondokana na umaskini kwa kuongeza kkipato chao. Kipato cha
mtu kinapoongezeka watoto wake watahudhuria masomo na kupata huduma bora za
afya. Wazee na akina mama nao watapata huduma bora za afya. Lakini kipato
hakiwezi kuongezeka kama mtu hataki kufanya kazi, hataki maendeleo, na hataki
kujishughulisha na kitu chochote. Maisha bora kwa kila mMtanzania yatapatikana
kama tutafanya kazi kwa bidii na maarifa. Inawezekana, kila mtu atimize wajibu
wake.
kaya ili watoto wahudhurie masomo na kwenda kliniki kupata chanjo na
huduma zingine za afya. Vile vile ongezeko la kipato litawezesha akina mama
wajawazito na wazee kupata huduma zote muhimu za afya.
Hivyo ndugu zangu natoa wito kwa wananchi wote watumie vizuri fursa hii
murua ya TASAF. Tushirikiane na uongozi wa TASAF kubuni miradi itakayotuletea
maendeleo ya haraka, miradi itakayoboresha huduma za jamii. Tushirikiane nao
kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo. Tuhakikishe kuwa tunafuata maelekezo ya
wataalam na viongozi wetu katika ngazi mbalimbali. Tuwafichue wabadhirifu wa
fedha za miradi ya TASAF na wale wote wanaotumia vibaya rasilimali za miradi.
Daima tukumbuke kuwa miradi hii ni kwa ajili yetu sisi pamoja na watoto wetu,
ndugu zetu na jamaa zetu. Tukifanya hivi nina imani tutakuwa na msingi imara wa
kujenga taifa linaloendelea na hatimaye kushinda vita dhidi ya adui watatu wa
maendeleo: umaskini, njaa na magonjwa.
Rai kwa Washirika wa Maendeleo na Viongozi wa TASAF
Mabibi na Mabwana;
Natumaini washirika wetu wa
maendeleo wataendelea kuunga mkono juhudi zetu hizi za kuondoa maadui watatu wa
maendeleo. Wamekuwa wakifanya hivyo tangu tulipoanzisha Mfuko huu wa TASAF na
nina imani wataendelea. Msaada wao utasaidia sana kufikia malengo yetu
tuliyojiwekea katika utekelezaji wa Awamu hii.
Nawaomba pia viongozi wa TASAF,
Kamati ya Taifa ya Uongozi, Menejimenti na Mkurugenzi Mtendaji waongeze ufanisi
na maarifa katika utendaji wao. Waongeze usimamizi wa fedha na rasilimali,
wajenge uwezo wa kusimamia utekelezaji wa miradi katika ngazi mbalimbali, na
wabuni vyanzo vingine vya kupata fedha za kuendeleza miradi. Naamini
wataweza.
Mwisho
Mheshimiwa Waziri;
Wageni waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Kabla ya kumaliza hotuba yangu naomba nitoe shukrani za dhati kwa Mhe.
Benjamin William Mkapa, Rais wa Awamu ya Tatu kwa kubuni wazo hili jema ambalo
manufaa yake tunayaona. Baada ya kusema hayo, sasa nipo tayari kufanya kazi
iliyonileta hapa Nazindua Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii kwa
matumaini makubwa kuwawamba sasa Watanzania sasa tumeupata ufunguo wa maendeleo
yetu sote. Napenda kutamka kwamba Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii,
(TASAF) umezinduliwa rasmi leo. Nawatakia kila la heri na mafanikio katika
utekelezaji wake.
Asanteni sana kwa kunisikiliza.kwa kutumia fursa ambazo mageuzi ya uchumi,
na usimamizi bora wa uchumi, umeweka mbele yetu.
Kwa pamoja tutafanya mengi. Na kwa mradi huu wa TASAF, ukichanganywa na
miradi mingine, na utaratibu huu wa kushirikisha wananchi katika shughuli za
kupunguza umasikini, ninaamini Watanzania wote tutakuwa na msingi imara wa
kujenga taifa linaloendelea na hatimaye kushinda vita dhidi ya umaskini.
Na sasa natangaza kuwa nimezindua rasmi Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo
ya Jamii (TASAF III).
Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.

No comments