Header Ads

ad

Breaking News

Hispania yaweka historia barani Ulaya


 *Yaichapa Italia 4-0

TIMU ya taifa ya Hispania, imekuwa nchi ya kwanza barani Ulaya kutwaa ubingwa wa maaifa ya Ulaya mara tatu mfululizo baada ya kuichapa Italia katika mechi ya fainali ya mataifa ya Ulaya iliyochezwa juzi, mabao 4-0 jijini Kiev, Ukraine.

Mabao yaliyowapa ushindi Hispania yalifungwa na David Silva, Jordi Alba, Fernando Torres na Juan Mata, mechi hiyo ilichezwa kwenye Uwanja wa Olimpiki jijini Kiev, Ukraine.
Mchezo huo ulikuwa tayari umetoa picha ya bingwa dakika 45 za kwanza, baada ya Andres Iniesta kumpasia pasi safi Cesc Fabregas aliyepiga krosi nzuri na kuunganishwa kwa kichwani kwa Silva dakika ya 14.

Dakika nne kabla ya mapumziko, Xavi  aliyewazidi ujanja wachezaji wa Italia, alimpasia mpira Jordi Alba ambaye hakufanya makosa, na kuifungia Hispania bao la pili.

Ilikuwa kitendo cha kushangaza kwa Mario Balotelli wa Italia, baada ya kumalizika kwa mchezo alikwenda moja kwa moja katrika vyumba vya kubadilishia nguo, huku juzudi za maofisa wa timu yake wakijaribu kumrudisha, kabla ya kurejea sehemu ya sheria.

Hata hivyo, , Italia  hawakuwa na hasira na walikuwa na matumiani ya kurejea kipindi cha pili na kusawazisha mabao hayo, mpaka  kocha Cesare Prandelli alipofanya mabadiliko kwa kumwingiza Thiago Motta na kumtoa Riccardo Montolivo , ambaye pia aliumia dakika nne baada ya kuingia na kutolewa, na kuwaacha wenzake wakicheza 10, dakika 30 zote.

Hatimaye, Hispani walikamilika kila idara na kuthibitisha  ni bora katika michuano hiyo. Wachezaji wanne wa kikosi hizo, Iker Casillas, Sergio Ramos, Andres Iniesta na Xavi, walistahili kutajwa wachezaji muhimu baada kuichezea timu yake mechi zote za Vienna, Johannesburg na sasa Kiev.

Wakati michuano hiyo ikiendelea, Hispania ilionekana kama dhaifu tofauti na michuano iliyopita.
Kocha Vicente del Bosque, alikataa kumtumia mshambuliaji wa kati, na kuendelea kuwapanga viungo wengi katika kikosi chake.

Kipindi cha pili, Hispania ilicheza tena pasi tano na kulifikia lango la Italia. Iker Casillas, Fabregas na baadaye Alba, aliyempasia Xavi aliyekuwa akisoma mchezo na kumsukumia mpira Alba, na kuukwamisha wavuni dakika ya 41 na kuwa bao la pili, huku kipa wa Italia Gianluigi Buffon akishindwa la kufanya.

Katika hali ya kawaida, Hispania haikuonesha kiwango kizuri, baada ya kuzidiwa na na Italia waliokuwa na asilimia 53.

Casillas alifanya kazi nzuri ya kuokoa mpira uliopigwa na Antonio Cassano na Balotelli akapiga shuti kali lililopaa juu ya lango la Hispania. Hakuna mtu atakayeweza kumhukumu kocha  Prandelli kwa washambuliaji wake kukosa mabao, Antonio di Natale alimajaribu kipa Casillas baada ya kupokea pasi kutoka Riccardo Montolivo ndani ya eneo la Hispania, lakini hakufunga bao.

Italia, ilipata pigo baada ya kumwingiza Motta, lakini alicheza dakika nne tu na kutoka akiwa juu ya machela na kuifanya timu yao kuwa katika wagumu kwani tayari walifanya mabadiliko yote.  

Torres alichukua nafasi ya Cesc Fabregas dakika ya 75, aliifungia Hispania bao la tatu dakika ya 84, bao lililowamaliza nguvu kabisa Italia, na bao la nne la kikosi hicho lilifungwa na Mata dakika mbili kabla ya filimbi ya mwisho.

Italia haikustahili, mechi ya mashindano makubwa kufungwa kwa mara ya kwanza na Hispania ilikuwa kwa penalti, tangu mwaka 1920 katika michuano ya Olimpiki. Hispania imevunja rekodi mara, sasa haijafungwa mechi 29 katika michuano hiyo.



No comments