SIMBA YAMUONGEZA MKATABA PROFESA MILOVAN
KLABU ya Simba ya Dar es Salaam imemuongezea mkataba wa
miaka miwili kocha wake Mserbia, Profesa Milovan Cirkovic baada ya kuridhishwa
na kazi yake kwa kipindi cha nusu msimu alichokuwa na timu hiyo tangu arithi
mikoba ya Mganda, Moses Basena.
Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ameiambia
BIN
ZUBEIRY jioni kwamba Milovan atakuwa kocha wa Simba kwa miaka miwili
zaidi tangu sasa baada ya kuongezewa mkataba.
“Kipimo cha mafanikio ya kocha ni mataji na soka safi, kitu ambacho
sisi kama viongozi tumekishuhudia Simba chini ya Profesa Milovan, sasa hatuoni
kwa nini tusimuongeze mkataba,”alisema Kaburu.
No comments