RAMBIRAMBI MSIBA WA PATRICK MAFISANGO
![]() |
Mafisango |
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha
mchezaji wa Simba na timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi), Patrick
Mafisango kilichotokea leo alfajiri (Mei 17 mwaka huu) kwa ajali ya gari
Dar es Salaam.
Msiba
huo ni mkubwa kwa familia ya mpira wa miguu kwani Mafisango kwa kipindi
chote alichocheza mpira hapa nchini akiwa na timu za Azam na baadaye
Simba, aliifanya kazi yake (kucheza mpira) kwa bidii.
Kifo
chake ni pigo kubwa si tu kwa familia yake na timu alizochezea, bali
ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Kati ambapo changamoto zake zilikuwa
dhahiri uwanjani.
Wakati
mauti inamkuta, Mafisango alikuwa ameitwa Amavubi kwa ajili ya mechi za
mchujo za Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika zinazochezwa mapema mwezi
ujao.
TFF
inatoa pole kwa familia ya Mafisango, klabu ya Simba, Shirikisho la
Mpira wa Miguu Rwanda (FERWAFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu
katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Mungu aiweke roho ya marehemu Mafisango mahali pema peponi. Amina
No comments