Miss Sinza 2012 kuanza mazoezi Juni Mosi
Na Mwandishi Wetu
MAZOEZI
ya warembo wataowania taji la Miss Sinza 2012 yamepangwa kuanza Juni
Mosi kwenye ukumbi wa Ten Star Lounge (Mawela Social Hall) ulipo karibu
na hotel ya Vatican City uliopo Sinza.
Mratibu
wa mashindano hayo, Majuto Omary alisema kuwa mazoezi hayo yataanza saa
10.00 jioni na ni ya wazi kwa warembo wenye nia ya kutaka kuwania taji
na zawadi nono za washindi wa mwaka huu ambao wataiwakilisha Sinza
kwenye mashindano ya Kanda ya Kinondoni, Miss Tanzania na baadaye katika
mashindano ya Dunia “Miss World”.
Majuto
alisema kuwa fomu za washiriki zitatolewa hapo hapo kwenye ukumbi wa
mazoezi na wengine wanaotaka kushiriki katika mashindano hayo wanatakiwa
kufika ofisi za Mama Tike Hair Fashion and Boutique zilizopo Sinza
Kumekucha kituoni, Ofisi za Miss Tanzania (Posta), ofisi za SMP zilizopo Kinondoni Mkwajuni, Brake Point (Kijitonyama na Posta) na kupitia mtandao wa balilemajuto.blogspot.com, sufiani mafoto.blogspot.com.
Alisema
kuwa kamati ya Miss Sinza kwa sasa ipo katika mikakati mbali mbali ya
kusaka wadhamini kwa ajili ya kufanikisha mashindano hayo yanayotarajiwa
kuwa bora kabisa mwaka huu.
“Tunaomba
wadhamini ikiwa ni makampuni, wafanya biashara, wadau wa masuala ya
urembo ambao wanataka kujitangaza kupitia mashindano haya kujitokeza
kusaidia waandaaji kwani lengo kubwa ni kuona Sinza inafanya mashindano
bora na yenye kuleta mafanikio makubwa kwa kutwaa taji la Miss Tanzania
na lile la Dunia,” alisema Majuto.
Alifafanua kuwa wameandaa
mikakati na mipango mbali mbali ili kuhakikisha Sinza mwaka huu inapata
mafanikio makubwa katika mashindano ya Miss Tanzania na yale ya Dunia.
No comments