Header Ads

ad

Breaking News

Kamati ya Utendaji ndiyo inamiliki tinu Yanga


                             Katibu Mkuu Yanga, Mwesigwa Celestine
WALE waliokuwa na mawazo kuwa utawala wa  uongozi wa klabu ya Yanga umevunjika rasmi baada ya  Mwenyekiti wake Llody Nchunga kujiuzulu, wamecheza pata potea kutokana na taarifa kuwa bado timu hiyo inamilikiwa na wajumbe wa kamati ya utendaji.
Shirikisho la Kandanda nchini (TFF) jana lilitangaza kuitisha kikao cha Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji  chini ya mwenyekiti wake Alex Mgongolwa kuangalia hatma ya klabu hiyo kufuatia kujizulu kwa wajumbe sita wa kamati ya utendaji.
Hata hivyo kikao hicho kilichokaa jana jioni kinaweza kujsindwa kutoa jibu lolote la kikatiba kutokana na ukweli kuwa kamati ya utendaji ya Yanga imebakiwa na wajumbe nane.
Wajumbe hao ni Tito Osoro, Sarah Ramadhan, Mbaraka Igangula, Mohamed Bhinda, Salum Rupia, Charles Mgondo, Maneno Tamba na Bosco Lingalangala.
Kikatiba wajumbe hao wanapaswa kukutana na kuchagua mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa muda huku zoezi zima likibakia katika mkutano mkuu wa wanachama uliopangwa kufanyika Julai 15 jijini. Hivyo hata taarifa kuwa timu ipo chini ya bodi ya wadhamini si za kweli kutokana na ukweli kuwa klabu hiyo kwa sasa haina bodi hiyo.
“Hii inatokana na ukweli kuwa wajumbe waliopo katika bodi hiyo ni wa kuteuliwa na kikatiba hawatambuliki kwani mpaka wakapitishwe na mkutano mkuu wa wanachama,” alisema mpasha habari wetu.
Idadi hiyo imetimia kutokana na taarifa kuwa baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji walitangaza kujiuzulu bila kuwakilisha barua kwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Mwesigwa Celestine huku wengine wakikanusha kuwasilisha barua na kudai kuwa ni za kughushi.
Mwesigwa alisema kuwa  hana barua ya kujizulu ya Igangula ambaye kwa sasa yupo Afrika Kusini kikazi. Alisema kuwa Igangula amempigia simu na kulalamika kuwa hajawahi kuandika barua yoyote ya kujizulu na kuweka nia ya kuwashitaki wale waliofanya zoezi hilo la kughushi mara akirejea.
Kamati ya utendaji ya Yanga inatarajiwa kukutana Jumamosi au Jumapili kujadili hatma ya klabu hiyo na uwenda ikachagua mwenyekiti  na makamu wa muda.

No comments