Didier Drogba awaaga wenzake kwa uchungu, atokwa na machozi
Mshambuliaji huyo hatari amesema inamuuma moyoni kufikia tamati ya miaka minane ya kuwa na Chelsea.
Drogba alizungumza huku analia wakati anawaambia John Terry, Frank Lampard na wengineo: ‘Hatutakuwa pamoja tena msimu ujao.’
Alitoa tamko hilo la kushitua katika sherehe za ubingwa wa Blues, saa 24
baada ya kuisaidia timu hiyo kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, anatarajiwa kuungana na mchezaji
mwenzake aliyekuwa naye Chelsea, Nicolas Anelka katika klabu ya
Shanghai ya China kwa mshahara wa pauni 200,000 kwa wiki.
Lakini uhamisho huo umeingia shaka jana usiku, baada ya kuibuka habari,
kocha Anelka amekwaruzana na wamiliki wa klabu hiyo ya Shanghai.
Drogba alisema: “Ingawa ni miaka mitatu sasa tangu niseme nataka
kuondoka, inaniwia vigumu kukubali nimefikia mwisho na klabu hii —
hususan tangu nikatae mwisho huu.”
Drogba aliliambia jarida la Ufaransa: “Nisingeweza kujiona nimekaa
benchi nawaangalia wachezaji wengine wanacheza, wakati klabu inapanga
kujenga timu mpya.
Anelka amesaidia mawasiliano kati ya Shanghai na Drogba kufikia sehemu n zuri.
Lakini Mfaransa huyo, hafurahishwi na hali ya mambo anayokabiliana huko
tangu avue dakluga zake na kukaa kwenye benchi la ufundi, akirithi
mikoba ya Jean Tigana mwezi uliopita na anaweza kuamua kuondoka.
No comments