Header Ads

ad

Breaking News

Waswaz kuchezesha mechi ya Simba dhid ya El Ahly Shandy



Patrick Mafisango akimpongeza Haruna Moshi Boban baada ya kufunga bao la pili dhidi ya JKT Ruvu. mwenye jezi namba 9 ni Gervais Kago

Na Mwandishi wetu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Swaziland kuchezesha mechi ya kwanza ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba na Al Ahly Shandy ya Sudan itakayochezwa Aprili 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Waamuzi hao wa mechi hiyo namba 71 ni Nhleko Simanga Pritchard atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake ni Mbingo Petros Mzikayifani na Sibandze Thulani. Mwamuzi wa mezani atakuwa Fakudze Mbongiseni Elliot.

CAF pia imemteua Kayijuga Gaspard wa Rwanda kuwa Kamishna wa mechi hiyo. Simba inatarajiwa kuingia kambini Jumatatu ijayo mara baada ya mechi yake ya ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Moro United.

Uongozi wa timu hiyo kwa sasa umeweka mkazo zaidi katika mechi dhidi ya Moro ili kuweka matumaini yake hao ya kutwaa ubingwa baada ya Yanga kulitema rasmi kombe hilo kufuatia kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar.

Yanga kwa sasa inawania nafasi ya pili pamoja na Azam FC, japo ina nafasi finyu sana kutokana na hali halisi ya timu hiyo kwa hivi sasa.

No comments