JKT RUVU, SIMBA ZAINGIZA MIL 30/-
![]() |
JKT Ruvu |
Pambano
la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya JKT Ruvu na Simba lililochezwa jana
(Aprili 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh.
30,095,000.
Jumla
ya watazamaji 8,362 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio
vya sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 15,000. Watazamaji 7,310
kati ya hao walishuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 3,000.
Baada
ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 4,590,762.71 kila klabu ilipata
sh. 4,455,551.19, uwanja sh. 1,485,183.73.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 1,485,183.73, Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 297,036.75 na Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 297,036.75.
Mfuko
wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 742,591.86, Baraza la Michezo
la Taifa (BMT) sh. 148,518.37 na asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh.
1,485,183.73.
Gharama
za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli
ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000 na nauli ya ndani kwa
mtathmini wa waamuzi sh. 10,000.
Mwamuzi
wa akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa kamishna, mtathmini wa
waamuzi na waamuzi sh. 120,000, gharama ya tiketi sh. 3,750,000,
maandalizi ya uwanja (pitch) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, usafi na
ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh.
2,000,000.
Gharama
nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu
ilipata sh. 585,340 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es
Salaam (DRFA) kilipata sh. 510,720.
No comments