Header Ads

ad

Breaking News

TTTA yaandaa mashindano Desemba


Kapsheni: Mikidadi Bunaya, akirudisha mpira wakati wa mazoezi ya tenisi kwenye Viwanja vya Gymkhana Dar es Salaam jana ikiwa ni maandalizi ya mashindano yatakayofanyika mwishoni mwa wiki.

 Chama cha Mpira wa Meza Tanzania (TTTA), kimeandaa mashindano ya Afrika Mashariki ambayo yatafanyika Desemba, mwaka huu Dar es Salaam.

Kocha Msaidizi wa timu ya taifa ya mchezo huo, Yahaya Mungilwa amesema wameamua kuandaa mashindano hayo ili kuendelea kukipa mazoezi kikosi cha timu hiyo, ili kukiweka sawa kukabiliana na mashindano yoyote yatakayowajia.

Amesema wanatarajia mashindano hayo yashirikisha nchi za Kenya na Uganda, lakini wakipata fedha za kutosha watazialika pia timu za Ethiopia, Rwanda na Burundi ili kuongeza hamasa na upinzani katika mashindano hayo.

Ameongeza kuwa timu hiyo ya taifa, tayari imepata mazoezi ya kutosha na bado wataendelea kujifua hadi wakati wa mashindano hayo, ili kujiweka vyema zaidi.

No comments