Header Ads

ad

Breaking News

Jamii yashauriwa kujiunga mfumo wa kisasa wa Push Obsever

JAMII imeshauriwa kujiunga na mfumo wa kisasa wa usimamizi wa vyombo vya habari wa kampuni ya Push Observer, ili kuweza kupata taarifa mbalimbali sahihi za kisiasa, kiuchumi, kibiashara na kiafya.

Wito huo ulitolewa na gwiji la masuala ya usimamizi wa vyombo vya habari, Bw. Joe Taylor kutoka Marekani, katika hafla fupi iliyowakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya habari, uchumi na biashara.
Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Push 
Observer, Bw. Omari Salisbury (kushoto)  na 
Joe Taylor wa Marekani

Bw. Taylor alisema kuwa, kila mtu anawajibu wa kujua mambo mbalimbali yanayohusu jamii na njia halisi ni kuputia mfumo wa kisasa (Digital Media Monitoring) ambao hurekodi na kuhifadhi taarifa hizo.

Alisema kuwa, mfumo huo umeenea sana nchi za Amerika na Ulaya na kuishukuru kampuni ya Push Observer kuanzisha utaratibu huo ambao pia, usaidia waandishi wa habari na wanafunzi.

Amefafanua kuwa, kwa wafanya biashara, mfumo huo ndiyo utawapa mwanga zaidi wa biashara zao kwani utawawezesha kujua mwenendo wa biashara yake, kujua mpinzani au mshindani anafanya nini katika soko husika.

Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Push Observer, Bw. Omari Salisbury akimshukuru Bw. Taylor kwa ujio wake na kutoa  mwanga wa mfumo huo ambao Tanzania haujaenea sana.

Bw. Salisbury alisema kuwa, tokea kuanzishwa kwa kampuni yake, mpaka sasa makampuni sita yamejiunga na yanafanya vizuri katika soko.

Amesema kuwa, wameamua kuanzisha kampuni hiyo ili kuiweka Tanzania katika ramani ya kisasa ya mambo ya usimamizi wa vyombo vya habari na kuwapa taarifa wadau masuala ya kijamii kuweza kupata maendeleo ya kisasa.

No comments